Video kwa hisani ya Prince MM
SHUHUDIA KWANZA VIDEO HIYO HAPO JUU KWA KUBOFYA 'PLAY'
WASANII WENGI WA BONGO WANA VIPAJI VINGI LAKINI BADO HATUJAWAENDELEZA AU KUWAWEZESHA VYA KUTOSHA.
MFANO MZURI NI KIJANA MUUMIN MWINYIJUMA (PRINCE) MWENYE SAUTI NA MVUTO NA KUJITUMA AWAPO JUKWAANI.
TUNAAMBIWA KUWA HATA INAWALAZIMU WASANII HAWA KUHAMA KUTOKA BENDI MOJA KWENDA NYINGINE KUTOKANA NA AMA UKIRITIMBA AU UBINYWAJI WA HAKI ZAO UNAOFANYWA NA WAMILIKI WA BENDI NA HATA BAADHI YA MAPROMOTA.
WAPO WANAOSEMA KUWA TATIZO LA KUHAMA HAMA NI TABIA TU YA MTU YA KUTORIDHIKA KWA HAO WASANII. WENGINE WANAONA SUALA LA KUHAMA WALA SI TATIZO BALI NI MAHANGAIKO YA KAWAIDA YA MAISHA YA BINADAMU KATIKA KUTAFUTA PENYE MALISHO YA MAJANI MABICHI ZAIDI!
TUTOE MAWAZO KUSAIDIA KUINUA VIWANGO VYA WASANII KWA FAIDA YAO NA TAIFA KWA UJUMLA!
______________________________________