Saturday, December 25, 2010

Merry Christmas & New Year
Wishing you all,
A Merry Christmas 
&
Prosperous New Year (2011)

Thursday, December 9, 2010

UHURU NA JAMHURI , 2010Poster design by:  wa- Chirangi

WATANZANIA
Tunapokumbuka 
na Kushereheka 
katika Siku-kuu  ya  
Uhuru na Jamhuri - 2010,
Nawatakieni kila la kheri na fanaka. 
Aidha nawahasa pia, tutumie muda huo kutafakari 
ni jinsi gani sote mmoja mmoja au katika Kikundi / Chama / Idara/ Asasi / Wizara tunaweka Mikakati ya kuimarisha Uwajibikaji na Uzalendo katika kutoa michango yoyote chanya kwa namna yeyote  inayokubalika kwa ajili ya kujiletea
Maendeleo ya kweli ya Mtanzania 
na Tanzania kwa ujumla.


Uhuru – kazi yetu !
Uhuru – kazi yangu!

Wenu,

Musuto wa- Chirangi

Thursday, December 2, 2010

My Better Half Graduates


Blogger Templates

 My Dearest Wife,  Marja Chirangi- Schoenmeker,

Congrats for the smart work on your studies in 
Public Health: Health Services Innovations 

The family is proud of you!
May you now continue to employ all what you acquired in terms of skills, knowledge and experiences in your medical practice as well as in whatever endeavors you engage in 
as applicable while giving quality services.


Love,

 Wa- Chirangi- Omwichukuru wa Nyamurugwa wa Kafwenyi

Wednesday, November 17, 2010

A New Health Centre in Musoma


Tumetangaziwa na Uongozi husika kuwa, Kituo cha Afya kipya kwa jina Bethsaida Health Centre, kilichoko katika kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma  kinaanza kutoa huduma za Afya kwa Wananchi kuanzia 17/11/2010.

Natoa wito kwa:
  • Watumishi wa Kituo hiki kipya,  kuwa wajitahidi kutoa huduma bora isiyo aghali huku wakitii taratibu ziongozazo na maadili ya Taaluma zao kwa moyo, nguvu na akili zao zote.

  •  Uongozi wa Kituo, kutumia kanuni za Menejiment bora na Mawasiliano yenye ufanisi  huku wakijali Watumishi wao na kutathmini shughuli kila wakati ili kuboresha kiwango na ubora wa huduma kwa Wateja.

  • Manispaa yetu  na Wananchi kwa ujumla kuunga mkono juhudi hizi kwa kukubali kuwa na makubaliano ya mkataba wa utoaji huduma kwa ushirikiano wa Serikali & Sekta Binafsi  (Public - Private Partnership)  ili kuwezesha kupunguza gharama za uendeshaji na hivyo gharama za matibabu kwa Wananchi.

Sote tunamshukuru Mungu na wote waliowezesha huduma hii kuwepo.  Aidha tunamkumbuka Mzee wetu Mutaragara (RIP), mtu wa watu ambaye eneo na nyumba yake milki ndipo kituo hiki kimejengwa.


********************************************


Tuesday, November 16, 2010

Eid Mubarak!


For this pictorial, credit to: Desert Peace- nicePakistan.comPaying Tribute to our beloved Grandma,

Kaka, Nyamurugwa wa Kafwenyi-Pili Binti Hussein(RIP),

our Uncle, Entrepreneur of the time in Musoma-township,

Rata, Juma Musuto Chirangi;(RIP)
Amri- Abeid Hse No. 21

&
Family,
Mai Nyasatu, Mai Nyamagoe (RIP)Cousins:-
Musa (RIP), Fatuma,Taabu, Mwanaisha, Said, Masatu, Meli (RIP):

I wish  all Muslims a blessing Festival of Sacrifice
(Eid al – Adha) as they commemorate the trials and triumph 
of Prophet Abraham. (Qur'an 16:120-121)

(namesake) wa- Chirangi
*******************************************************
*******************************************************

Wednesday, November 10, 2010

Tusipiganie Fito

 Picha: Kwa hisani ya Michuzi-Mzee wa Libeneke.

Uchaguzi umekwisha, Rais J.Kikwete ameshaapishwa tayari kuunda na kuongoza Serikali kwa kipindi cha miaka 5.  

Pamoja na matukio ya hapa na pale,  Mimi na familia yangu tunawapongeza Watanzania wote kwa jinsi mlivyoendeleza amani wakati wote wa Kampeni hadi kukamilika kwa Uchaguzi  Mkuu. 

Tunamwombea Rais, Makamu wake Mh. M.G.Bilal, Mawaziri na Viongozi Wengine wote wa Mihimili ya Taifa katika ngazi zote, afya njema, maono na uongozi  wenye ufanisi katika Nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

Niliguswa sana na kauli ya "Tusigombee Fito", hivyo nami natoa mwendelezo wa wito huo kuwa :

'Shime Watanzania wote, pasi kujali tofauti zetu za ki-itikadi na vyama vyetu vya siasa, tutafute fito za kutosha na tusaidiane ili kujenga nyumba yetu kwa ushirikiano.'


Tanzania itajengwa na Watanzania Wenyewe.
Mungu ibariki Tanzania.


Wakatabhau,

Judy, Marja & Musuto wa- Chirangi

**********************************************************
**********************************************************

Kaka Umefanya Kweli!
Kaka, Godfrey Chirangi Mutaragara Chirangi wa- Muhongo wa- Nyawayega wa Rihu,

Tunakupongeza sana katika kuhitimu  kwa kufaulu  vyema Masomo ya Shahada kutoka Chuo Kikuu cha Mount Meru katika fani yako ya Ualimu na Lugha ya Kiingereza.
Mwenyezi Mungu azidi kukujalia wewe, mkeo Jane na wanao wote katika maisha. Aidha tunakuombea ili yumkini uendelee kutoa huduma bora kwa Wananchi wa Tanzania kwa ufanisi zaidi.


"Do not ask if a man has been through college; ask if a college has been through him; if he is a walking university" - Edwin Hubbell Chapin.


Ni sisi,
Judy, Marja & Musuto Chirangi 
************************************************
************************************************

Thursday, October 14, 2010

In Memory of Mwl. J.K.Nyerere (1922 - 1999)To date Baba wa Taifa letu, Mwl. J.K.Nyerere, (RIP) still speaks to us. We as Tanzanian, MUST refuse vehemently to be divided, neither on tribal lines nor on religious rivalry.

My tympanum as well as my heart continues to acknowledge his public articulation and what he stood for.


In his honour, please click here: http://www.britishpathe.com/record.php?id=42256  and play the video.


Credits to the British Pathe for achives of such documentaries were our generation is also able to flash back to the glimpse of jubilation, our Nation's founding Fathers and Mothers experienced.wa- Chirangi

Monday, September 20, 2010

Matumizi Holela ya Msimu 'Chakachua'
Utangulizi
 Chakachuliwa,  ni msamiati nyumbulifu (derivative word) toka neno mzizi chakachua  uliotumika katika mijadala Bungeni na sasa pia waandishi wa habari kueleza hali ya mafuta (dizeli & petroli) yaliyochanganywa na vimiminika vingine kama vile mafuta ya taa, maji n.k ili kuongeza ujazo kwa ajili ya kujipatia faida zaidi baada ya mauzo (kwa bei ile ile) ya bidhaa hiyo iliyoteremshwa thamani ulinganisha na uhalisia wake.
 Sina hakika kama neno hili linatambuliwa rasmi na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ambalo kisheria ndilo lenye mamlaka ya kuratibu shughuli za uundaji wa istilahi za Kiswahili. Wala si yakini kama utafiti wa kina umefanywa na Taasisi yeyote yenye ithibati kama vile TUKI juu ufafanuzi wa dhana iliyobebwa katika istlahi hii kutoka lugha chanzi na hatimaye uundaji wa kisawe hicho cha chakachua.  Mpaka hapo itakapoelimishwa vinginevyo, neno hili nalichikulia kama kisawe kisicho rasmi katika lugha ya Kiswahili.


Eneo Stahiki Kiteminografia
Kwa kuzingatia mbinu ya kiteminografia (terminography), hili neno chakachua linastahili zaidi  kuonekana katika Kamusi ya Istilahi ya Sayansi-Fani ya Kemia hususani kwenye somo la taitresheni (titration) ambapo kuna uchambuzi wa matokeo ya uchanganyaji wa vimiminika tofauti sanjali na udhibiti wa ujazo wake.
 Maana & Kusudi
Kuchakachua  ni udanganyifu kwa kusudi la ama ki- biashara katika kutafuta faida kubwa kwa njia isiyo halali au kwenye upimaji (tests) ambapo matokeo fulani yanalazimishwa ama yaonekane au yasionekane kinyume na hali halisi. Mara nyingi kuna njia kuu tatu za udanganyifu katika vimiminika kama vile:-
 1.      Adulteration –  ughushi kwa kuongeza vimininika au kuchanganya na vitendanishi  (reagents) duni
2.      Dilution   - uchujuaji kwa kuongeza zaidi maji
3.      Substitution – kibadala, kwa kuongeza kimiminika mbadala.   

Matumizi ya neno
Pamoja na changamoto katika lugha yetu ya Kiswahili ya kuwa na upungufu wa istilahi anuwai katika uwanja wa Sayansi na Teknolojia, hivi  karibuni, neno kuchakachuliwa  limetumika kama msimu katika medani za siasa na kijamii kwa ujumla katika tamathali za semi na kwa mapana kama sinonimi (synonym) ambapo  istilahi moja ya Kiswahili inahusishwa na dhana zaidi ya moja katika lugha chanzi. Ndiposa neno hili limeweza kutumika kubeba dhana kadha wa kadha hadi kuleta mikanganyiko, kama vile kughushi, kubadilisha, kutotenda haki, kuharibika, kudanganya, kubatilishwa (mfano, leo nimesikia mtangazaji akisema kuwa “Ratiba ya ligi kuu imechakachuliwa”) n.k,  na hata –enye utata,  (mfano mtu anasema, “Alipata mchumba aliyechakachulika”akimaanisha mchumba mwenye utambulisho tata) n.k
 
Pendekezo
Ningekuwa na uwezo wa kushawishi BAKITA, ningependekeza kuwa kisawe rasmi kinacholandana na dhana nzima ya kupunguza uthamani wa kimiminika kwa kuchanganya na kitu kingine kiwe  kuchukuchua  badala ya kuchakachua. Kwamba neno mzizi liwe chukuchua ambalo linaweza kutoholewa kutoka chukuchuku mf. mchuzi chukuchuku  ambao ni mchuzi mwepesi usio na thamani inayoridhisha, mchuzi uliowekwa maji mengi (omusosi omujubhe) kupita kiwango kitakiwacho  hivyo mafuta yaliyochukuchuliwa ni mafuta yasiyo katika kiwango kitakiwacho ni mafuta yaliyoonhezwa kimiminika kingine na kushusha ubora wake.
  
Nathubutu kusema,


Musuto wa- Mutaragara wa- Chirangi
Verbal Diarrhoea Dehydrates Human Dignity. Chirangi, (2000)(Shukrani kwa Blogu ya barclayp yenye picha)

Thursday, September 16, 2010

TUPULIZE VUVUZELA

Video: Vijanazaidi -You Tube. Shukrani kwa Kikwete 2010 Campaign Team & Michuzi:


Tanbihi: Nisemalo hapa laweza lisiwafurahishe wengine lakini linabaki kuwa kweli:

  • SANAA ILIYOUNDWA INA WELEDI WA HALI YA JUU . 
  • MAVAZI YALIYOTUMIKA NI YA HESHIMA NA YAMELANDANA NA JAMII (WANA CCM) HUSIKA PAMOJA NA SHUGHULI ILIYOPO
  • STAILI MPYA ILIYOONESHWA (KIDUKU) IMEKONGA NYOYO
  • MATUMIZI YA VUVUZELA NA RANGI ZAKE YANANYANYUA HISIA ZA MWAFRIKA KATIKA SHUGHULI ILIYOFANA HUKO BONDENI
  • MELODI YA MARLAW KAMWE HAISHAWISHI HASIRA BALI UTULIVU, MBEMBELEZO NA MGUSO WA MWILI NA ROHO
  • UCHAGUZI WA MANENO KATIKA WIMBO UNAHAMASISHA WANACHAMA NA PIA UNATUMA CHANGAMOTO KWA WANACHAMA WA VYAMA VINGINE
  • USHIRIKI WA  NGUVU WA VIJANA KWA HIYARI NA MUZIKI WA KISASA TANZANIA NI UBUNIFU NA FURSA ILIYOTUMIKA NA TIMU YA KAMPENI KWA UMAKINI KATIKA KARNE YA LEO!

WAHUSIKA WOTE WANASTAHILI PONGEZI!

NINACHOWEZA KUSHAURI TU NI KUWA,
NAFASI YA MADANSA WA KIKE INGEWEZA KUBORESHWA KWA KUWAPA MUDA WA UWIANO NA WALE WA KIUME JUKWAANI.

Saturday, August 21, 2010

WOSIA KWA WAHITIMU WA 2010 KISARE NURSING SCHOOL

Vitabu katika Maktaba ya Kisare Nursing School
Wapendwa Wahitimu,
Kisare Nursing School,
Mugumu, Serengerti,

Sanjari na kuwatunuku Wahitimu vyeti husika, mara nyingi inapofika siku ya mahafali mengi yanasemwa na kuimbwa katika ama kuwapongeza au kuwahasa kama siyo kuwaangaliza katika majukumu yatakayowakabili katika jamii.

Turuhusuni nasi leo tuwatunuku nukuu chache zinazohusika na KUPATA ELIMU kama tafakuri mtakazozibeba katika fikra zenu kama zilivyoanikwa na magwiji katika nyanja na tasnia mbalimbali kama ifuatavyo:-

 “Vitabu vyaweza kuwa hatari, vile vyenye uzuri wa hali ya juu, ni vema vikawekewa tahadhari isemayo, Onyo, hiki kinaweza kubadilisha maisha yako”. Helen Exley .


 “Vitabu na maandiko yote ni tishio kwa wale wanaonuia kuiminya kweli.”
Wole Soyinka.


 “Upo utofauti kati ya mwenye ari atafutaye kusoma kitabu na asiye na ari atafutaye kitabu cha kusoma”. Gilbert Chesterton


 “Kusoma ni nauli yenye unafuu kuelekea kokote”. Mary Schmich.


 “Elimu yetu inatakiwa kutupa chanjo ya kujituma kwa ajili ya jamii nzima na kuwasaidia wanafunzi kukubali yale yanayokubalika kwa ajili ya maisha yetu ya mbeleni”. Baba wa Taifa, Mwl. J. K. Nyerere


 “Elimu ni siraha ya nguvu kubwa unayoweza kutumia kuibadili dunia”. Nelson Mandela.


 “Mizizi ya elimu ni michungu, lakini matunda yake ni matamu”. Aristotle.


 “Wakati mnaondoka hapa (Chuoni), msisahau kwa nini mlikuja hapa”. Adlai Stevenson
Masomo yenu hapa yanaweza kuwa yamefika ukingoni,
lakini kumbukeni kuwa kuelimika kunaendelea daima!
Wahitimu, Wakufunzi, Watumishi na Wadau wengine wote
hongereni sana na tunawatakieni kila la kheri.


Wenu,

Judy, Marja & Musuto Chirangi
Uholanzi, July, 2010.

Friday, August 20, 2010

MFANO WA MWANA DIASPORA SHUJAA

“…Why should my face not look sad when the city where my fathers are buried lies in ruins, and its gates have been destroyed by fire?" Nehemiah 2:3

MISINGI 10 ALIZOTUMIA MWANA DIASPORA SHUJAA


1. Kuwa na mawasiliano endelevu na nyumbani kujua si tu habari za kifamilia lakini pia maisha ya jamii na maendeleo yao kwa ujumla.
2. Kuwa na mzigo na matatizo yaliyoko nyumbani.
3. Kumshirikisha Mola katika mipango na mafanikio yetu.
4. Kutumia fursa na rasilimali tulizo nazo kwa ajili ya maendeleo ya jamii yetu
5. Kufanya tathinini za kisayansi za matatizo / mahitaji yetu halisi na kuweka mipango kazi na mikakati.
6. Kuhamasisha wengine na kugawana majukumu ikiwezekana kwa kujali vipaji / uzoefu / uwezo wetu.
7. Kushiriana pamoja kutekeleza mipango kazi.
8. Kutokuyumbishwa wala kukatishwa tamaa na wanaotubeza na au wanaotaka kutuondoa katika maono na mwelekeo wetu wa ki-maendeleo.
9. Kuonyesha ushujaa, kujilinda na ikibidi kupambana na wale wanaotaka vita na sisi.
10. Kusimamia haki, maadili na kuwajali wahitaji zaidi.

Kanuni hizi nimezinyambulisha nilipomkumbuka Kiongozi - shujaa mmoja katika Agano la kale, aliyeitwa Nehemia.

TAFADHALI KAMA HUJAWAHI SOMA AU KUTAFAKARI KWA UNDANI KITABU CHA NEHEMIA WAKATI NDIO SASA!
N.B Hata katika misaafu mingine kama Koran na hali kadhalika Hadith kuna mashujaa na wanamapinduzi wengi tu kama Nehemia.

Kwa kifupi tu ili kukupa hamu ya kusoma,

 Nehemia alikuwa mshika kombe (the Cup- bearer) wa Mfalme wa Uajemi. Pamoja na kuwa katika maisha mazuri huko ughaibuni na katika hiyo kazi ya watu wachache sana katika ‘special branch’, katika kuwasiliana kwake na nyumbani, alipata habari kuwa kuta za Yerusalemu & malango yake vimebomolewa na kuchomwa moto.
 Alibeba mzigo wa taabu zilizokuwa zinawakabili watu wa nyumbani Jerusalem, akahuzunika na kuomboleza sana.
 Akamwomba Mola juu ya jambo hilo
 Akatumia nafasi yake kumwendea Mfalme ambaye alimpa ruhusa na kumpa usalamana pia vitendea kazi vya kuanzia kazi ya ujenzi. (Sisi tunatumiaje vipawa na nafasi tulizo nazo kuendeleza jamii zetu?)
 Alipofika kabla ya kuanza kazi alifanya tathmini ya kiwango cha uharibifu na kazi iliyotakiwa kufanywa na kupanga kazi.
 Akahamasisha wenzake na kuwaambia kuwa tujenge pamoja, kazi iligawanywa vyema kufuata uzoefu/ uwezo. Mfano Makuhani walipewa kushughulia mlango waliouzoea na kuufahamu – mlango wa kondoo!
 Watu walishirikiana wakachapa kazi mchana na usiku
 Kuliibuka akina Sanbalati, Tobian na wenzao wakawabeza na kutaka kuwaondoa kazini, lakini Nehemia alisisitiza kuwa hawezi kuacha kazi.
 Maadui walipopanga njama, ulinzi mkali uliwekwa na wakapambana nao. (Ni aibu sisi leo tunakatishwa tamaa wala hatupambani na maadui wetu katika maendeleo!)
 Nehemia aliwasimamia haki kama kuwasaidia maskini n.k na pia akawawajibisha wakiukaji ili kulinda maadili yaliyokubalika.

Hitimisho:


Yawezekana tukawa na maisha bora zaidi popote tulipo nje ya mji au nchi, inatubidi kubeba mzigo na kuhuzunika na hali yoyote mbaya (kama ipo) katika jamii zetu. Mbele ya Viongozi wetu au Mashirika yenye uwezo au yeyote mwenye uwezo wa kutusaidia kutatua tatizo lililopo, tunapaswa kusema kuwa,
“Tutakosaje kuwa na huzuni wakati mji/ nchi ya baba zetu na mama zetu ina hali isiyoridhisha?”
Halafu tufanye kweli kwa tuchukuwa hatua 10 za kuleta maendeleo kama kiongozi wa mfano Nehemia alivyofanya.

Verbal Diarrhoea Dehydrates Human Dignity. Chirangi (2000).

Tuesday, August 3, 2010

UGONJWA WA TAFSIRI NJE YA MAZINGIRA (Contextomy)


 Zao la Sanaa hiyo hapo juu ni vazi-potosha liloundwa nami mwenyewe kuonyesha jinsi ugonjwa nyemelezi wa Tafsiri nje ya mazingira yake (Contextomy) unavyoweza kuwa na athari katika kupotosha umma. 

Pata chanjo yake mapema kwa kutafakari jambo katika mazingira yake na katika ukamilifu wake!

Tuesday, July 20, 2010

Wahubiri katika sauti zenye Mpangilio

Kwanza Bofya kwenye play button ya Redio hapa chini usikilize.
Miziki ya kumsifu na kumtangaza Mungu imekuwepo tangu enzi za agano la kale na inaendelea kukua kwa kasi katika mapigo,ghani na staili kadha wa kadha za uchezaji wa Waimbaji.

Umuhimu wa nafasi ya muziki katika Makanisa, Misikiti na Masinagogi ni mkubwa sana katika kusaidiana na Wahubiri wengine kufikisha ujumbe kwa hadhira inayokusudiwa.

Aidha Kwaya ziimbazo au zipigazo miziki ya Kiroho pia kama  walivyo mawakala wengine wa mabadiliko ya mwanadamu, zimefanya kazi kubwa ya kuwabadili, kuwafariji, kuwahubiri, kuwashawishi,  kuwafundisha, kuwaonya na hata kuwapagaisha wanadamu wengi, mimi nikiwa mmoja wao!

Ukiachilia wasanii au kwaya ambazo zimeshapiga hatua kubwa, Wahubiri hawa wa sauti zenye mpangilio wanakabiliwa na changamoto nyingi, hapa chini leo nataja mbili tu:- 

1. Kuhakikisha kuwa ujumbe wao unahaririwa na kupangwa vyema kabla haujawafikia hadhira. (si kujali tu mipangilio ya midundo na staili za kuruka)

2. Kurekodi kazi zao na kuwa na hati miliki. Wengi wametunga nyimbo na baada ya muda zimeachwa na kupotea tu bila kutunzwa, hapa namkumbuka Mwalimu wangu Julius Zabuloni Machumu (RIP), ambaye hadi mauti yake hakuwahi kurekodi kazi yake ya usanii iliyokuwa na ubunifu wa hali ya juu enzi hizo za miaka ya 80. Kati ya vibao vyake vilivyotikisa katika makambi ya kiroho ni  Katondo tondo Maryamu Nemuka, Isaka, Kinachoshangaza, Jerusalem, Paliondokea Yohana Mbatizaji n.k 

Wito:
Wadau wote tujifunge vibwebwe kuwasaidia Wahubiri hawa kwa kadiri ya uwezo wetu na vipawa vyetu  maana utume wao na jumbe zao ni za muhimu sana katika maisha yetu leo na kwa vizazi vijavyo.


Hapa chini ni picha ya Mwalimu mzoefu wa Kwaya ya Upendo ya Kanisa la Mennonite Tanzania Mugumu,  ndg. Gemma Igira (mwenye shati nyeupe) akiwa na Mwalimu mwenzake gwiji katika muziki wa injili ndani ya Studio yenye wapishi wa muziki waliobobea ijulikanayo kama Studio Habari Maalum  Mwanza wakati waliporekodi Album ya Upendo Choir kwa jina la Tenda Miujiza. Heshima kuu kwa Waalimu wote waliotoa msaada mkubwa, Wanakwaya wote walioshiriki kutoka Jimboni kwao chini ya uongozi wa jimbo wa Mchungaji  Wilson Shanyangi Machota.  .

Ukipenda kujipatia nakala yako ya Album hiyo ambapo kibao hicho hapo juu (SIFUNI) kimo ndani wasiliana moja kwa moja na Uongozi wa Kwaya ya Upendo au Uongozi wa Jimbo (KMT- Mugumu c/o S.L.P 17 Mugumu, Serengeti, Tanzania au tuma barua pepe kwa gemma.igira@hotmail.com.
Monday, May 17, 2010

‘Huduma za Uuguzi zinazokidhi Viwango; Wauguzi Kuongoza katika Huduma juu ya Magonjwa Sugu)’TAFAKURI YA KAULI MBIU KWA WAUGUZI NA 
WATUMISHI WENGINE WA AFYA MKOANI MARA

KATIKA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI
(INTERNATIONAL NURSES DAY) 12 MEI, 2010

‘Huduma za Uuguzi zinazokidhi Viwango;
Wauguzi Kuongoza katika Huduma juu ya Magonjwa Sugu)’
IMEANDALIWA NA KUWASILISHWA NA :

Dr. Chirangi, Bwire, (MPH)

I. Utangulizi

Wageni waalikwa Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kiserikali na yasiyo ya kiserikali, Viongozi wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Wapendwa Mashujaa wa Taaluma nyeti – Wauguzi wa Tanzania,

Paukwa…., Pakawa!

Madaktari walipokuwa wamekamilisha kazi zao, wamechoka bin taabani na kupumzika, ule wakati ambapo ukimya na giza totoro vimetawala miongoni mwa wagonjwa majeruhi vitandani, yeye aliweza kuonekana akiwa peke yake na ki-taa chake mkononi akipita kuwazungukia wagonjwa na kuwahudumia ipaswavyo..Florence Nightingale (12 May 1820 – 13 August 1910)Habari ndiyo hiyo, iliyoleteleza mtaalamu na shujaa - Florence Nightingale, kutambulika aka mama mwenye taa (a lady with the lamp) katika kutoa huduma ndani ya hospitali ya kijeshi (Scutari hospital) huko Uturuki wakati wa vita (Crimean War) kama ilivyonukuliwa katika gazeti (Times newspaper) la Alhamis 08 Februari 1855.

Kutokana na ushujaa wake katika kufuata wito na vipawa vyake vilipomsukuma, kutokana na moyo wake wa huruma kwa wagonjwa, kutokana na uongozi wake wa mipango, kutokana na utendaji wake wa kimaadili na usafi wa kiwango cha juu, kutokana na umahiri wake katika kutunza takwimu, kuzitafsiri na kuziwasilisha kwa ajili ya kuboresha mfumo wa afya, kutokana na kuitetea na kuiboresha taaluma ya Uuguzi, Baraza la Kimataifa la Wauguzi (The International Council of Nurses kwa kifupi ICN) liliamua tuwe tunashereheka kwa kutambua mchango mkubwa wa Wauguzi wote katika Afya na Maendeleo ya jamii zetu kwa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya shujaa wetu Florence kila tarehe 12 Mei.

Tunaipongeza ICN kwa kazi yake makini ambapo huandaa si tu kauli mbiu ( bali pia nyenzo za utekelezaji wa kauli mbiu kwa kila mwaka. Aidha nawashukuru pia Chama cha Wauguzi Tanzania kwa kazi kubwa ya uratibu kuhusiana na maendeleo ya Taaluma ya Uuguzi na pia kutukutanisha hapa leo kama iliyo kiada, wataalamu wanapowasha ile taa na kujikumbusha kiapo cha maadili ya taaluma ya Uuguzi na zaidi ya yote kutafakari mipango mkakati juu ya mada husika ya mwaka katika maboresho ya Afya ya Mtanzania.


II. Magonjwa Sugu Utekelezaji wa Kauli Mbiu ya mwaka 2010
Mwaka huu Wauguzi wanapiga mbiu juu ya utoaji wa huduma za Uuguzi katika jamii zinazokidhi viwango na kuhakikisha kwamba Wauguzi wanashiriki kikamilifu katika huduma dhidi ya magonjwa sugu / sindika (delivering quality, serving communities:
Nurses leading chronic care)

Ndugu, Wauguzi wataalamu wenzangu katika huduma za afya, tukumbushane kuwa kwa mujibu wa takwimu za WHO (2005), magonjwa sugu kama vile Saratani, Pumu, Kiarusi, Shinikizo la Damu, Unyongofu (msongo wa mawazo), Kisukari n.k ndio yanasababisha asilimia 60% ya vifo vyote ulimwenguni.

Aidha kama tunafuata nyayo zake malaika wa huduma (the Ministering Angel)- Florence, katika kuwa makini na takwimu na kuzitumia katika kuboresha afya zetu, basi sote tutashirikiana kwa kuelimisha jamii kuwa ni hoja potofu isiyo ya kisayansi, kudhani kuwa magonjwa hayo sugu yanawakabiri zaidi watu wa nchi zenye kipato cha juu (matajiri). WHO (2005) inaonyesha takwimu za wazi kwamba 80% ya wagonjwa ni wale walio katika nchi za kipato cha chini na kati (Low & Middle income countries), hivyo Tanzania ni mojawapo!

Wengi wetu tumejifunza kwa namna moja au nyingine juu ya hayo magojwa kwa undani na tutaendelea kupata elimu juu ya matokeo ya tafiti mbalimbali kuhusu kinga, matibabu na au huduma kwa wagonjwa husika. Hapa niruhusuni nidodose tu kidog kwa nini udhibiti wa magonjwa sugu ni mada nyeti na jukumu la watu wa Mataifa yote pasi kujali utofauti wetu katika nasaba, jinsia, umri, kipato, imani wala itikadi za kisiasa .


Ni bayana Magonjwa sugu, yanatugharimu uhai wetu. bila kuchukuwa hatua, inakadiriwa kuwa jumla ya watu wapatao milioni 17 watakufa dunianii, mwaka huu kutokana na maradhi sugu.

Kwa vile magonjwa sugu ni ya muda mrefu na yenye uhitaji wa huduma za muda mrefu, maradhi haya yana madhara hasi makubwa `kwa nchi kiuchumi na kijamii. Maana yanafisha nguvu kazi katika uzalishaji na kuongeza matumizi makubwa serikali na familia husika katika kuyathibiti. Magonjwa haya yanasababisha watu kushindwa kufikia malengo yao maishani. Kuna gharama zisizo za moja kwa moja (indirect costs) kama upotezaji wa rasilimali muda makazini, mashuleni na hata majumbani n.k

Kuongezeka kwa magonjwa sugu duniani kunatokana na sababu kadha wa kadha zikiwemo ya mabadiliko ya kijamii, utandawazi, kuenea kwa maisha ya mijini (urbanization) pasipo utoshelezaji wa miundo mbinu na huduma kwa wote, kuongezeka kwa idadi ya wazee na hata ubinywaji wa haki na fursa sawa kwa wote katika mapato na huduma.III. Utekelezaji wa Kauli Mbiu ya mwaka 2010

Kwa mujibu wa Maadili ya jumla ya Uuguzi kama yanavyoainishwa na ICN – Code of Ethics, Wauguzi wana wajibu wa msingi wa kushiriki katika kuimarisha afya na kuzuia maradhi. Aidha tunakubali kushirikiana na jamii kwa ujumla kuanzisha na kuunga mkono shughuli zinazostawisha afya na mahitaji ya kijamii ya umma.

Ndugu zangu haitoshi kutambua na kulalama juu ya changamoto mbalimbali zinazotukabili leo katika taaluma ya Uuguzi nchini. Ni vyema kwa kutumia elimu, ujuzi na umoja wetu ndani ya Chama cha Wauguzi Tanzania, Vikao vya Wauguzi na Uongozi katika Vituo vya Afya husika, Bodi za Afya za Wilaya na Mikoa na hata kupitia Kitengo cha Huduma za Uuguzi katika Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, tuwasilishe matatizo yetu na mapendekezo yanayotukabili kwa hoja zenye takwimu rejea zilizotafsirika kisayansi kama Muasisi wetu, Meneja, Mtakwimu, Mkufunzi, Mshauri na Muuguzi mwana maboresho Florence alivyofanya katika kuipa Taaluma hadhi yake, kuwajengea uwezo Wauguzi na kuleta mapinduzi chanya ya mfumo katika huduma za Afya.

Shime, tushirikiane na wadau wote wa afya katika maeneo yetu kutekeleza Mpango Mkakati wa tatu katika sekta ya afya (the third Health Sector Strategic Plan) 2009 – 2015 ambao uko sanjari na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millennium Development Goals) kufikia 2015 .
Tushirikiane kuelimisha umma juu ya vidokezo hatarishi vya magonjwa sugu na pia sisi wenyewe kama watumishi wa idara ya afya tuwe mfano (model) wa kuigwa katika familia zetu, makazini kwetu na katika jamii zetu kwa ujumla katika namna tunavyoishi kuboresha afya zetu; mfano:
 Kuepuka uvutaji wa sigara / tumbaku
 Kuepuka unywaji wa pombe uliokithiri
 Kupata lishe bora kwa wakati muafaka
 Kufanya mazoezi
 Kuepuka ngono sisizo salama
 Kudhibiti muendelezo wa msongo wa mawazo nk

Katika kutoa huduma husika kwa wakati muafaka kwa wagonjwa, wa magonjwa sugu, tunashauriwa kutumia CCM ( the Chronic Care Model)  ambapo tunaunda mfumo:-
wenye mgojwa aliyehamasika na mwenye taarifa kamili, anayejiamini na kuweza kufanya maamuzi juu ya afya yake nauwepo wa timu ya Wataalamu ambao pia wana taarifa kamili juuu ya ugonjwa, maamuzi na mahitaji kwa ajili ya kutoa huduma kwa kiwango cha juu kwa kushirikiana na taasisi za afya.

Na pia kufuata ushauri wa WHO- ICC Framework, 2002 ( WHO-Innovative Care for Chronic Conditions , mkakati ambao pia unasisitiza kufanya maamuzi kwa rejea za takwimu, kulenga jamii husika, kuzuia ugonjwa, huduma bora iliyoratibiwa vyema,uwezo wa kuiga na kutumia kinachofaa kufuatana na mazingira husika na kuwa na ushirikiano miongoni mwa Wataalamuna na kuungwa mkono na jamii katika huduma zitolewazo.


III. Hitimisho

Ndugu Wauguzi na wageni wote waalikwa tofauti na siku kubukizi nyingi tulizonazo nchini, katika siku ya Wauguzi duniani hatukutani kwa sababu tu ya kusherehekea bali tunakutana kutafakari juu ya uratibu na utekelezaji wa mpango mkakati katika kutimiza kauli mbiu yetu ya mwaka husika.

Kwa moyo wa upendo, ninasajiri shukrani zangu za dhati kwa mchango mkubwa wa kipekee unaotolewa na Wauguzi popote walipo ulimwenguni hata ambapo Madaktari na Wataalamu wengine wanakuwa wamechoka bin taaban na giza totoro likitanda ama katika kumpunguzia mwanadamu maumivu au kurejesha na kuboresha siha yake au kumkarabati au kumtunza au kumwelimisha na kumshauri juu ya hamasa na utetezi wa maisha ya afya njema, kinga na au tiba ya maradhi.

Tutakiane kila la kheri tunapowasha taa zetu katika kuhamasisha mabadiliko chanya ya mifumo yetu na jamii kwa ujumla kuelekea huduma bora kwa wote na maisha yenye siha bora dhidi ya maradhi sugu yanayotukabili.Sunday, January 3, 2010

Kumbukumbu ya Baba Chirangi Rubhoja Bhanu

'WALIGA ULI-RUBHOJA BHANU'

Tarehe 03, Januari, 2010 inakamilisha takribani miaka mitatu tangu ututoke ghafla.
Familia yako na Wanahistoria tunaendelea kukukumbuka kwa mengi uliyotufundisha kwenye njanja mbalimbali katika Uongozi, Uadilifu na Wema wako.

Katika kumbukumbu hii, dhamira zetu leo zinaguswa zaidi na tabia yako isiyokifani ya
UKARIMU ULIOKUWA NAO KWA WATU WOTE PASI KUJALI MAKABILA, ITIKADI ZA KISIASA, IMANI, JINSI, UMRI WALA HALI ZAO ZA KIUCHUMI.

Aidha haikuwa ajali Wanadamu wakati wa ujana wako wakakupa majina ya utani kama vile Rubhoja Bhanu na pia Nyamulila Mwirango utambulisho ulioashiria tabia hii ya kukarimu watu uliyoionyesha kwa vitendo pasipo uzandiki wala masharti kwa manufaa binafsi.

Tunamuomba Mola azidi kutukumbusha nasi leo kuwakarimu wageni na wahitaji kwa jinsi tunavyoweza kuwasaidia maana kwa kufanya hivyo si tu kuwa tutakuwa tunaenzi kauli mbiu
uliyoipenda ya Haki Huinua Taifa bali pia tutakuwa tunawajibika kuwasaidia wenzetu wenye mahitaji mbalimbali kama tunavyotakiwa katika kujali utu na haki za kila Binadamu.


KWA HESHIMA NA SHUKRANI, FAMILIA YA CHIRANGI INAWASILISHA.

Friday, January 1, 2010

HERI YA MWAKA MPYA 2010Ndugu zangu Watanzania,


Huku wengine tukiwa tumetengana kwa milima, mabonde, bahari, mipaka ya nchi na umbali mrefu na tukiwa katika mazingira tofauti kiutamaduni na kijiografia
nawatunuku nyote katika jina liletalo umoja na matumaini ya maisha.“Mwenye matumaini hukesha usiku hadi auone mwaka mpya bali
asiye na matumaini hukesha ili kuhakikisha kuwa mwaka unapita”.

("An Optimist stays up to see the New Year in, a Pessimist waits to make sure the old one leaves ")
Ama tuwapo Watumishi au Wanafunzi, kauli hii niliyoinukuu ya busara ya
Bill Vaughan inatugusa sote ikituhasa kuwa, tunapoingia katika mwaka mpya wa 2010 tuwe watu wa matumaini.

Pasi uzandiki sote tunapewa changamoto ya kuwa na matumaini katika:

1. Kuweka mipango na kuimarisha uongozi wetu katika kazi na katika familia zetu
2. Kutoa huduma bora zaidi kwa Wateja wetu
3. Kujifunza kwa bidii stadi anuwai zenye ufanisi katika kutatua matatizo yetu
4. Kujenga na au kuboresha Umoja na Amani katika Taasisi na kwa Taifa lote.


Ninawatakieni afya njema, kila la kheri na fanaka tunapofungua sura ya kwanza na kuanza kuiandika katika hiki kitabu kipya cha 2010.


Wakatabhau,


Musuto wa- Chirangi
Utrecht, Uholanzi,