Sunday, January 23, 2011

RIP Justice Mapigano

H.E, President Kikwete pays his last respect to the late Justice Dan Mapigano (RIP), retired Judge of the High Court of Tanzania; laid to rest yesterday on 19/01/2011
Familia yote ya marehemu Jaji Mapigano na rafiki yake wa karibu sana, Baba Prof. Muhongo (pichani) nawapa pole na kuwaombea faraja itokayo kwa Mola.    


(Picha kwa hisani ya Michuzi)


Monday, January 17, 2011

Maisha ya Mwanadamu Simulizi la Mola; BISEKO (RIP)
Ndg. Biseko - Master (kwenye nyota) akisikiliza kwa umakini taarifa ya Wagonjwa na Tiba katika kikao cha Asubuhi cha Watumishi wa Afya- Nyerere DDH kabla ya kuuliza maswali ambayo mara nyingi yaliibua  ama changamoto, udadisi na au utafutaji wa
utoaji Huduma bora zaidi za Afya kwa wagonjwa!
Monday, January 3, 2011

UVUMILIVU NA SUBIRA CHANGAMOTO TOKA KWA BABAKUMBUKUMBU (4) YA MZEE A. MUTARAGARA CHIRANGI

Pamoja na Mwanafalsafa Friesrich Nietzsche (1844 - 1900) kuona na kusema kweli kwamba, kuwa na subira au uvumilivu ni ngumu sana, hata kwa Washairi Wazamivu kushindwa kuzuia hasira zao kutoa  dhamira ya ushairi wao au kwamba shauku haitasubiri!,

 Tulimsikia na kumwona baba Mzee Mutaragara Chirangi (RIP), akionyesha uvumilivu katika anga za Siasa kwa hali isiyotegemewa.Ni siku nyingine tena leo, ikiwa imetimia takribani miaka minne tangu atutoke duniani, tunaendelea kupata kumbukizi la changamoto toka maisha ya  huyu mzee wetu.

Katika anga za ki- Siasa hususan baada ya chaguzi, uwezo wa Binadamu wengi kuweza kuvumilia au kunyenyekea au kuonyesha subira au kujizuia kusema au kufanya jambo ambalo halina tija wala maendeleo ya mwanadamu kwa leo na kesho, ni mdogo sana.

Dhamira ya uvumilivu aliyoitangaza mzee Chirangi kwa vitendo, kamwe haikumaanisha kushindwa kudai haki au kupigia debe maisha ya kukosa misimamo, la hasha;  bali uwezo wa kutulia baada ya uchaguzi na kuchambua hali halisi na kuchukua hatua muafaka pasi jaziba,  husuda wala chuki zisizo na maana.

Wenye kumbukumbu, wanaelewa ni mara ngapi mzee huyu aliwahi kugombea nafasi mbalimbali katika njanja kadha wa kadha, akashindwa na miitikio yake ilikuwaje na hata pia ilipotokea akashinda alisema na kufanya nini kwa waliokuwa washindani au hata wapinzani wake.

Hebu tusome sehemu tu ya moja ya Hotuba zake aliyoitoa Agosti 1987,baada ya kutoa huduma kwa mfululizo wa miaka 15 kama Mwenyekiti wa CCM  Musoma mjini. Nanukuu:

Kama ambavyo nimekuwa nikisema na kutenda, ieleweke wazi kuwa kiongozi achaguliwaye kwa kutoa fedha, ataongoza kwa kuchukua fedha, vilevile achaguliwaye kwa kufuata ukabila, atasimamia kabila, naye yule achaguliwaye kwa kampeni moto toka juu huenda akaondolewa kwa kampeni baridi kutoka chini.
Aidha, ni kitendo cha kutokukomaa kisiasa, kujenga chuki na hasira kwa mtu yeyote eti kwa sababu ya kutokupigia kura, kukushinda kwenye uchaguzi au kuazimia kugombea nafasi uliyodhani umetengewa wewe pekeke”.Japo umelala baba, sauti  na maisha yako yataendelea kutufunza milele na milele.
Kwa kila jambo kuna majira yake.....!


Musuto wa – Chirangi
Kny. Familia Yote
03/01/2011