Thursday, December 27, 2012


Wishing You All 

a Happy, Peaceful and Successful 

 New Year - 2013 

Sunday, December 9, 2012



Watanzania wote,


Tutakiane siku njema ya tunaposherekea miaka 51 toka tupate Uhuru wetu (Tanganyika).
Tuzidi Kuwajibika na sote tuwe Wazalendo juu ya maendeleo ya nchi yetu.


Kila mtu akiwajibika kwa nafasi yake tunaweza.  



Friday, September 21, 2012

Uko wapi usalama wa waandishi wa habari wawapo kazini



Uko wapi usalama wa waandishi wa habari wawapo kazini
Hili lilikuwa swali la Kipindi cha ITV cha Malumbano ya Hoja la tarehe 20/09/2012

Nami naona maeneo manne ya muhimu kwa usalama wa Mwanahabari: 

1.    Mwanahabari mwenyewe:  NO STORY IS WORTH YOUR LIFE." So pull out before it's too late.   Awe na stadi za msingi za kujilinda inapobidi, asijisababishie hatari (kuripoti uongo, kuchafua wengine kwa uongo au mambo yasiyo na tija katika jamii) na awe na kitambulisho kinachoonekana(inapostahili), na  vifaa vya kujilinda (protective gears) awapo kwenye eneo la vurugu / hatari.      
               
2.    Mwajiri / Mhariri mwandamizi: lazima afanye utafiti wa eneo la kutolea habari (risk assessment) kabla hajamtuma mwandishi kama ni mahala pa hatari na awe na mawasiliano ya moja kwa moja na utayari kumwokoa endapo kuna shida. Wanahabari wote lazima wawe mikataba mizuri ya ajira, bima ya afya na maisha. Majukwaa na vyama vya Waandishi wa habari pia viko katika kundi hili kuhakikisha kuwa maisha ya Mwanahabari hayako hatarini na kwamba anafanya kazi yake kwa kufuata maadili ya kazi yake na kwa uhuru 

3.    Mihimili ya dola (Bunge, Serikali na Mahakama): Vyote vinapaswa kumlinda Mwanahabari kama ilivyo kwa raia wote kwa Bunge kutunga sheria bora, Serikali kusimamia sheria, kanuni na taratibu na mahakama kutafsiri sheria na kutoa haki. Polisi ni chombo cha dola hivyo kinapaswa kutimiza wajibu wake kwa haki na kuwafikisha wakosaji mbele ya haki bila kutumia nguvu zisizo za lazima.

4.    Raia wote: kwa kuthamini mchango wa mwanahabari popote na kuwapa ushirikiano

Nawapongeza ITV kwa kuanzisha mijadala kama hii kwa uwazi.

Nawasilisha;


Wa- Chirangi

Friday, August 31, 2012

Udanganyifu katika Mitihani - Swali la kipima joto


Jawabu la kukabili udanganyifu katika mitihani ya shule za msingi liko katika kuhakikisha kuwa tunakuwa na mfumo endelevu wa utoaji na usimamizi wa elimu bora na tathmini yake kuanzia Wizarani hasi Shuleni (a sustainable and effective quality assurance system of education). Mfumo huu lazima uangalie inputs zote yaani rasilimali-wanadamu (Waalimu, Watumishi wengine & Wanafunzi), sera, mitaala, miundombinu, vitendea kazi na pia michakato (processes) na bila kusahau stadi katika usimamizi wa mitihani (examination administration).


wa - Chirangi

BURIANI MAMA BERTHA KIFUTU


Kwa huzuni, tunapotafakari kututoka kwa ghafla kwa mpendwa Mama yetu Bertha Kifutu, tunaendelea kukumbushwa kuwa kifo si kutoweka kwa mwanga wake, bali kuzimwa kwa taa yake wakati wa mapambazuko baada ya kukamilisha safari ya maisha yake hapa duniani.


Ingawa Mwandishi, Hans Christian Andersen, alitukumbusha kuwa, maisha ya Mwanadamu ni hadithi  isimuliwayo kwa ukamilifu na Mola, turuhusuni nasi tusimulie japo kwa kudodosa rejea ya maisha ya huyu Mama yetu japo kwa aya moja, kama Mithali ya Mfalme Solomoni Mwana wa Daudi inavyosimulia;
Kwamba, Mwanamke mwema, kwa mikono yake, hufanya kazi zake kwa nguvu na Wanawe humwita Mbarikiwa, pia huamka kungali giza (asubuhi na mapema), kuangalia mambo ya nyumbani kwake, wala hali chakula cha uvivu; hivi ndivyo ilivyokuwa pia kwa huyu Mama yetu, Sengi Nyamambala wa Makanya hadi mauti ilipomkuta asubuhi na mapema (katondo- tondo muruguru) akiwa mfano wa Mama aangaliae mambo ya nyumbani kwake na kutunza familia!

Hakika, ingawa kifo kinatuondolea wapendwa wetu, kamwe hakiwezi  kutuondolea fikra na matendo yao ya kishujaa. Aidha, kwa vile huacha katika kumbukumbu zetu, alama za upendo zisizofutika kwa jinsi walivyoshirikiana nasi, basi tumuombe ndg. Sira, Kiongozi wa iliyokuwa kwaya yake (Imani - Choir), Kanisa na Jamii kwa ujumla, tuendeleze hamasa na jitihada za mpendwa wetu katika kuishi maisha ya kumtukuza Mungu wetu kwa furaha.

Swali kuu la kujiuliza; je, sisi tumempa Mungu kipi cha ziada kuturuhusu kuingia katika kumbukumbu za Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi leo tarehe 26/08/2012, ilhali makucha ya mauti hayakutoa nafasi hata ya siku mbili tu wala kwa familia ya mpendwa wetu kuweza hata kusikiliza tamko lake au kuagana naye?


Katika huzuni twaomboleza, katika huruma twawafariji wafiwa, katika tafakuri twajihoji juu ya maisha na uhai wetu- swali lisilojibiwa hata na Wana-Baijirontolojia (Biogerontoligists) wazamivu wanaotafiti namna ya kurefusha miaka ya kuishi uzeeni!

  
Pamoja nanyi katika maombolezo,



Judy, Marja & Musuto wa Mutaragara wa Chirangi

Saturday, May 5, 2012

Hongera sana Prof. Muhongo


SOTE TUNAMPONGEZA PROF.DR.S. MUHONGO KUTEULIWA NA RAIS KUWA MBUNGE NA PIA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI.
Kuteuliwa kwako kuwa Waziri katika Wizara nyeti ya  Nishati & Madini ni kiashiria cha wewe kuwa Mwajibikaji, Mwaminifu na mwenye Elimu & Ujuzi husika. Baba & Mama Hongereni sana.
 
 Tunakutakia kazi njema kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Thursday, March 1, 2012

WEDDING E- ALBUM

  


We wish the family of Mr. Mrs. Dr. Bwire & Violeth Chirangi all the best in their marriage life. 

Wholeheartedly we appreciate the good work performed by their preparatory wedding committee led by Mr. Abbas Chamba



Thanks to all  (family members & friends) who contributed towards that dazzling wedding!

Much gratitude to all the photographers, designers and the wedding e- album with the link below. 
 http://www.blurb.com/books/3023307

Saturday, February 25, 2012

WAJINA WA BIBI NYAMURUGWA - PILI BINTI HUSSEIN AHITIMU SHULE


TUNAMPONGEZA BINTI WETU  (MTOTO WA DADA GRACE) AITWAYE PILI KWA KUHITIMU  MASOMO YAKE YA SEKONDARI HUKO KENYA KATIKA SHULE YA KUJA SPECIAL SECONDARY SCHOOL FOR DEAF.

MOLA AMJALIE YALIYO MEMA KATIKA KUSOMA ZAIDI  KWA AJILI YA MAENDELEO YAKE , YA MAMA YAKE, YA FAMILIA NA TAIFA KWA UJUMLA .

AIDHA TUNAWAPONGEZA WAALIMU WAKE WOTE HUKO DAR ESLAAM NA PIA RONGO, KENYA.



Blogger Templates

Tuesday, January 10, 2012

PROF. MUHONGO ATUNIKIWA TUZO NYINGINE YA KIMATAIFA













Kwa mara nyingine tena  Prof. Sospeter Muhongo alitunukiwa  Tuzo ya Kimataifa ya Kisomi ya Mfalme Napoleoni ijulikanayo kama    'Ordre des Palmes Académiques (Order of Academic Palms)' toka Serikali ya Ufaransa. Hii ni kutokana na mchango wake wenye ufanisi duniani katika medani za  
Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
 
Tunampa pongezi  na kumwombea azidi kutoa huduma zake za kiwango cha juu kwa Watanzania na duniani kote kwa ujumla. 




























Wasifu wake kwa muhtasari ni kama ifuatavyo:

ABRIDGED CURRICULUM VITAE

Nationality:
Tanzanian

Language:
Fluent in Reading, Speaking & Writing English, Germany, Swahili & French (Basic)


Visionary Leadership – Excellent Management Skills – Transparency – Innovation –Efficiency - High Impact Delivery

PROFESSIONAL PROFILE:
Professor.
A full Professor of Geology- University of Dar Es Salaam (UDSM), Tanzania since 2001 and Honorary Professor- University of Pretoria, South Africa. Recognised for teaching excellence, dedicated to intellectual honesty. Head of Geology Department of UDSM (1997- 2002), with emphasis on training & research quality assurance.

Executive Director.
The founder and first Executive Director (2007- 2010) of the International Council for Science – Africa, Region, Provided strategic, transparent leadership with a yearly budget of more than US$. 870,000 for de- novel scientific projects, conferences and high-demand policy development ventures for Africa.

Professional Fellow & Consultant
A Member of the International Experts Group of OECD, Vice-President for Commission of the Geological Map of the World, Fellow of eight highly professional societies including the Geological Society of London and Chinese Academy of Geological Sciences. Undertaken over 100 scientific research, consultancy services & Chaired Conferences in mineral industry, environment, sustainable energy, including the     UN-Economic Commission for Africa, AU- Commission and UN-International Year of Planet Earth. 

Scientific Researcher, Scholarly Writer and Editor
Undertaken numerous field researches on Mineral Exploration, Geological Mapping and Laboratory tests in African, Europe & USA. The Editor-in-Chief of the Journal of African Earth Sciences and Associate Editor of Precambrian Research . Author or co-author of over 150 Scientific articles and Technical papers.

SELECTED AWARDS AND RECOGNITION:
Recipient of numerous scholarly and professional awards, grants and fellowships including:
2007, Honors Award, Geological Society of South Africa on Meritorious contribution to the Earth Science Profession, 2006, Tanzanian National Award (TAST Award) for Outstanding Research in Science & Technology, from the Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH), 2004, first recipient of Robert Shackleton Award for Outstanding Research in the Precambrian Geology of Africa.

FORMAL EDUCATION:
1985 - 90
Technical University of Berlin, FRG
Dr.rer.nat.
1983
University of Dar Es Salaam
M.Sc. Geology
1980- 82
University of Gőttingen, FRG
M.Sc. Research
1976 -79
University of Dar Es Salaam
B.Sc. (Hons) Geology




Mr. & Mrs Dr. Bwire & Violeth Chirangi

"Love does not consist of gazing at each other, 
but in looking together in the same direction".  
 ~Antoine de Saint-Exupery



As from the 3rd of Dec  2011, Dr. Bwire & Violeth wholeheartedly, declared in public to be 'looking in the same direction' as they exchanged their vows at The Kanisa La Mennonite Tanzania, Musoma.  

May our God be upon their blessed marriage life. 





Blogger Templates