Saturday, December 30, 2017

Asanteni Sana WanaCCM 2017





 Wanachama wa CCM;  Rafiki  na ndugu zangu;

 Asanteni sana kwa kunitia moyo na kunifanya kuwa Mgombea Uwenyekiti CCM Mkoani Mara.

"Mpira wangu waweza kuwa umegonga nguzo ya goli; lakini bado upo uwanjani ; bado upo mchezoni"

Ada ya mja hunena Muungwana ni  kitendo.  Kwa kila jambo na majira yake. Tutakiane Kheri katika mwaka mpya wa 1918.

Tuesday, March 22, 2016

REST IN PEACE - COMRADE SOSPETER KONGOLA KARAMBA




BURIANI KAMARADE SOSPETER  KONGOLA WA KARAMBA

Kwa mara nyingine tena, kauli isiyobadilika wala kuulizwa ya Mola wetu pale Bustanini Edeni, akinena “….hakika mtakufa” imetimia:  Tarehe 18/03/1016, mauti imezuru katika familia ya Karamba!   
Kwa butwaa na huzuni mkubwa, tulipokea taarifa hiyo iliyobeba simanzi tokana na kifo cha Kijana Sospter  Kongola akiwa katika matibabu huko Dar es salaam.
Ewe Mauti ya Mwili kamwe, hutaweza kutuondolea kumbukumbu ya ushirika usio mipaka na huduma njema zenye umilisi na adala ya mtu wa watu, mdogo wetu Kongola.
Tunakiri kuwa kifo huleta simanzi, lakini imani husababisha fikra tunduizi za maisha baada ya maisha ya hapa duniani. Pale ambapo, tunasema ni mwisho wa maisha ya kiwavi, hakika ni mwanzo wa maisha ya kipepeo! Japo amekufa, mdogo wetu ameanza maisha mapya!
Ewe kifo, waweza kusababisha mtanziko; tena una uwezo wa kuitenga miili yetu lakini kamwe huwezi kuzitenga roho zetu; huwezi kuzifuta hisia zetu,  kumbukumbu za maisha wala picha isiyofutika ya tabasamu la Kongola lililoashiria ushirika wake katika jamii.
Tunamkumbuka kwa mengi ya kutufunza sisi ambao bado tunaendelea kujaliwa nafasi ya kuishi hapa duniani.  Sosy  atakumbukwa kwa ucheshi na kujenga mahusiano na watu wengi  huku akiwapa misaada mbalimabli iliyokuwa ndani ya uwezo wake.  


Tunakiri kuwa:  “KIFO HUACHA MAUMIVU YA MOYO, HAKUNA AWEZAYE KUYATIBU,
 BALI UPENDO HUACHA KUMBUKUMBU, HAKUNA AWEZAYE KUIIBA”. KOMREDI SOSY KONGOLA,  KATIKA KUSANYIKO HILI LENYE SIMANZI, UPENDO WETU KWAKO UMETUACHIA  KUMBUKUMBU ISIYOIBIWA AMBAPO TUNAENDELEA KUKUPIGIA SALUTI TUKIENZI CHAPA  ULIZOTUACHIA KATIKA SAFARI YA MAISHA YAKO HAPA DUNIANI.

PENGINE WENGINE WATAELEZA MENGINE YANAYOJIKITA KATIKA MAPUNGUFU YAKO KAMA BINADAMU AMBAYO HATA WAO WANAYO;  SISI  TUTAENDELEA KUELEZA  NA KUJIFUNZA NA KUYATUNUKU MAISHA YAKO YA:-

Ø  UCHESHI NA  UTANASHATI ULIOTUKUKA MAHALA POPOTE, KILA WAKATI ,
Ø  URAFIKI  NA USHIRIKA MWANANA  KWA WATU WENGI PASIPO MIPAKA ISIYO NA TIJA,
Ø  UTUMISHI WAKO HODARI  KAMA MFANYAKAZI  KATIKA IDARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII  ULIYEAJIBIKA KWA MAADILI YA UTUMISHI WAKO,
Ø  USHIRIKI WAKO KWA VITENDO KATIKA SHUGHULI ANUAWI ZA SIASA, MAENDELEO YA KIJAMII NA  KIUCHUMI.
Si maandishi wala machozi yetu, yanayoweza kuonyesha kwa ukamilifu  huzuni tuliyo nayo moyoni mwetu kwa kuachwa na mpendwa wetu. Nawasihi tumuenzi Kongola kwa kuiga yale mema aliyoyatenda katika jamii.
Wana Familia, Jamaa, Marafiki,Wana – KMT, Wana CCM na wafiwa wote kwa ujumla poleni sana kwa msiba huu.
Faraja kuu na mioyo ya subira iwe nasi sote toka kwa Rabuka wetu hata katika mwamba huu tusioweza kuupanda kama Zaburi 61:2 ituelekezavyo:  
“Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.”
Tunawapa pole wafiwa wote kwa msiba huu mkubwa.

Buriani Sosy, Buriani Komredi Kongola.


Dkt.  Musuto wa Mutaragara wa Chirangi
Mmoja wa Rafiki Wengi wa Kongola.

Friday, November 6, 2015

KILA LA KHERI, SOTE TUSHIRIKIANE KUFANYA KAZI TU!





Baada ya kula viapo stahiki, mbele ya Jaji Mkuu;tunamtakia 
Rais na Amiri Jeshi Mkuu wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.  John Pombe Joseph Magufuli kila la kheri katika majukumu hayo makubwa na ya juu nchini kwetu. 
Aidha sote tunabaki na wito wa kuweka kando tofauti zetu na kudumisha umoja wa kitaifa huku tukifanya kazi kwa bidii na uadilifu kwa ajili ya maendeleo yetu na Taifa letu kwa ujumla.

Thursday, October 29, 2015

Hongera Prof. Dkt. S. Muhongo - Mbunge Mteule


Tunampongeza Prof. Dr. Sospeter Muhongo (Ordre des Palmes Académiques), Kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Mbunge katika Jimbo la Uchaguzi la Musoma Vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25/10/2015.

Kwa uelewa na mapenzi ya wananchi wa Jimbo lake wakizingatia Kauli Mbinu yake:

 'TUKUZE UCHUMI ;TUONDOE UMASKINI PAMOJA'

Wananchi wameongea kupitia sanduku la kura.

Tunamtakia kila la kheri katika uwakilishi wa Jimbo na katika kulitumikia Taifa kwa ujumla.
Tuna imani naye katika uwajibikaji wa kweli katika kukuza uchumi kwa maendeleo ya Watanzania wote. 

Shukrani za kipekee, zimfikie Mkewe, Mama yetu, Bibi Bertha Muhongo (Msc, MBA), Timu nzima ya Kampeni na wote walioshiriki katika kufanikisha ushindi huu, hususan Wapiga Kura - Wananchi wa Musoma Vijijini. 





Saturday, October 24, 2015

SHUKRANI KWA WANANCHI: OMWAKA GWO OBHWATASYO NA IMPOKOCHOLE.


Kama ambavyo niliendelea kufanya toka tarehe 01/08/2015; naendelea kuwashukuru kupitia blogu yangu  watu  wote walioniunga mkono na hata ambao hawakuniunga mkono kwa namna moja au nyingine katika Kura za Maoni katika nafasi Ubunge Jimbo la Musoma Mjini.

Waweza sikiliza na kudadavua zaidi kwa kujikumbusha vionjo vya 'Omwaka gwo Obhwatasyo na Impokochole' hapa:










Maisha yanaendelea, hata baada ya Uchaguzi!
Tanzania Tubaki kuwa Kisiwa cha Amani! 


wa- Chirangi, PhD

Monday, June 22, 2015

Dr. Chirangi urges Nurses to serve with competence & integrity

Musuto wa Mutaragara wa Chirangi, akiwapa Wosia Wahitimu na Wadau wa Taaluma ya Uuguzi  katika Chuo cha Sayansi za Afya - Kisare; Serengeti.