Thursday, October 29, 2015

Hongera Prof. Dkt. S. Muhongo - Mbunge Mteule


Tunampongeza Prof. Dr. Sospeter Muhongo (Ordre des Palmes Académiques), Kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Mbunge katika Jimbo la Uchaguzi la Musoma Vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25/10/2015.

Kwa uelewa na mapenzi ya wananchi wa Jimbo lake wakizingatia Kauli Mbinu yake:

 'TUKUZE UCHUMI ;TUONDOE UMASKINI PAMOJA'

Wananchi wameongea kupitia sanduku la kura.

Tunamtakia kila la kheri katika uwakilishi wa Jimbo na katika kulitumikia Taifa kwa ujumla.
Tuna imani naye katika uwajibikaji wa kweli katika kukuza uchumi kwa maendeleo ya Watanzania wote. 

Shukrani za kipekee, zimfikie Mkewe, Mama yetu, Bibi Bertha Muhongo (Msc, MBA), Timu nzima ya Kampeni na wote walioshiriki katika kufanikisha ushindi huu, hususan Wapiga Kura - Wananchi wa Musoma Vijijini. 

2 comments:

Anonymous said...

Jembe hilo liko tayari kulima sawia popote! Mimi namkubali sana huyu mtu maana ni mchapa kazi.

Mkama said...

"Truth be spoken.....kwa lugha ya wenyewe; au Mnyonge mnyongeni Haki yake Mpenzi"; Huyu Professor wa ukweli sana, NINAMKUBALI SANA. HONGERA SANA PROF. Katende kwa kasi na ujasiri ili kuendelea kujitofautisha na M_Professor Titles/Position/Vyeo. UBARIKIWE.