Sunday, June 19, 2011

SIKU YA AKINA BABA DUNIANI
Katika siku ya leo ya Akina Baba Duniani (Fathers'day)
 (Jumapili ya tatu ya mwezi Juni)

Niseme neno baba, kumbukizi la maishayo!

Swali lako kwangu, akili ilotathminika, 

Ndiyo yako kwangu, kibali kisofutika,

Hapana yako  kwangu, kinga ilosikika,

Kofi lako kwangu, tabia ilokarabatika,

Utanashati wako kwangu, hamasa ilosimika,

Saa yako kwetu, standadi ilotumika, 

Mzani wako kwetu, msawazo usofichika,

Mpango wako kwetu, andalizi lilorekodika,

Msimamo wako kwetu, kipimo kisotetereka,

Ukarimu wako kwetu, kifani kisosahaulika,

Niseme neno Baba, kumbukizi la maishayo!