Tuesday, November 8, 2011

Engaged

 
Dr. Bwire Chirangi & Miss. Violeth  Kessy

As you are engaged; 
We wish you all the best  and God's blessings
towards your 
Wedding  Day
 

Friday, July 29, 2011

BURIANI WA ASK. BUTENGÉ

B
Azikwa Musoma, tarehe 27/072011.

BURIANI ASK. MSTAAFU SALMON SARIGE BUTENGÉ
Uwepo wa utulivu mahala hapa ni heshima, tafakuri na kujihoji wakati tunapata rejea ya safari ya maisha ya Mtenda-kazi wa Bwana, Ask. Salmon Sarige Butengé  japo kwa dakika moja.
Ewe kifo, unaweza kuitenga miili yetu lakini kamwe huwezi kuzitenga roho zetu, huwezi kuifuta miguso wala kumbukumbu za maisha ya Wapendwa wetu.
U wapi mauti  na machungu yako?  Hatukuongelei tena kwa kuwa umaarufu wako ulishafunikwa  na  Ufufuo  na Tumaini alilotuachia Bwana wetu Yesu Kristo.
Kama hamasa toka kwa Bibi Mahalia Jackson ilivyomgusa Mch. Martin Luther King, Jnr, na hatimaye kuteremsha mistari ya karne “Nina njozi” (I have a dream), ndivyo tulivyoweza kushuhudia  hamasa  ya kishujaa, isiyomungúnya maneno ya mama  yetu,  Bibi Ask.  Lois Sarige Butengé  akinena,
"Yaika! wa Butengé, yaika!",  katika kadamnasi hususan wakati wa Makambi pindi  Mchungaji  / Askofu Butengé  alipokuwa akitema cheche za injili mathalani  juu ya  somo la Mtenda-kazi wa Bwana au Maji yaliyo hai n.k, huko Mugumu, Bumangi, Majita, Mugango, Musoma, Nyabange, Shirati, Mwanza, Dar es salaam na kwingineko.
Ee Mola, kama huko Mbinguni pangehitajika Mkutano wa Kiroho, tusingesita kutamka kuwa Mjoli wako Salmon Sarige uliyemtwaa ni mmojawapo wa Rasilimali-Binadamu mwenye taranta husika.
Bwana umetwaa, Jina lako linaendelea kubarikiwa na bila shaka mwangwi wa sauti ya mama Lois, sasa imepokelewa na malaika wakiimba,
"Gendelela okwaika wa Buteng’e, gendelela okwaika! "
Wana Familia, Jamaa, Marafiki na Wana – KMT kwa ujumla poleni sana kwa msiba huu.

Ni sisi

Judy, Marja & Musuto  wa- Chirangi.
Utrecht, the Netherlands
26 Julai, 2011

Sunday, June 19, 2011

SIKU YA AKINA BABA DUNIANI












Katika siku ya leo ya Akina Baba Duniani (Fathers'day)
 (Jumapili ya tatu ya mwezi Juni)

Niseme neno baba, kumbukizi la maishayo!

Swali lako kwangu, akili ilotathminika, 

Ndiyo yako kwangu, kibali kisofutika,

Hapana yako  kwangu, kinga ilosikika,

Kofi lako kwangu, tabia ilokarabatika,

Utanashati wako kwangu, hamasa ilosimika,

Saa yako kwetu, standadi ilotumika, 

Mzani wako kwetu, msawazo usofichika,

Mpango wako kwetu, andalizi lilorekodika,

Msimamo wako kwetu, kipimo kisotetereka,

Ukarimu wako kwetu, kifani kisosahaulika,

Niseme neno Baba, kumbukizi la maishayo!

Saturday, April 23, 2011

MBARAKA WAKATI WA PASAKA

                                                                                                                                    Easter 2011

Saturday, February 26, 2011

TUNATOA POLE

 



TUNATOA  POLE NA FARAJA KWA FAMILIA ZILIZOPOTEZA WANAFAMILIA WAO NA WALE WOTE WALIO ATHIRIKA MOJA KWA MOJA TOKANA NA AJALI YA
MILIPUKO YA MABOMU TOKA MAGHALA YA KIKOKSI CHA JWTZ CHA 511
GONGO LA MBOTO TAREHE 16/02/2011.

WATANZANIA NA RAFIKI ZETU WOTE TUENDELEZE JUHUDI ZA 
KUTOA MISAADA MBALIMBALI KUWASAIDIA WOTE WALIOPATWA 
NA  HAYA MAAFA NA UHARIBIFU WA MALI NA WANYAMA WAO.

AIDHA NI MATUMAINI YETU KUWA, BAADA YA UCHUNGUZI KUKAMILIKA, WANANCHI WATAELEZWA TAARIFA KAMILI NA PIA HATUA MUAFAKA KUCHUKULIWA IKIWA NI PAMOJA NA ZILE ZA KUPUNGUZA MAZINGIRA HATARISHI YANAYOWEZA KUSABABISHA MILIPUKO MINGINE TENA YA NAMNA HIYO 
NA AU MADHARA KWA WANANCHI NA MALI ZAO.

Sunday, January 23, 2011

RIP Justice Mapigano

H.E, President Kikwete pays his last respect to the late Justice Dan Mapigano (RIP), retired Judge of the High Court of Tanzania; laid to rest yesterday on 19/01/2011
Familia yote ya marehemu Jaji Mapigano na rafiki yake wa karibu sana, Baba Prof. Muhongo (pichani) nawapa pole na kuwaombea faraja itokayo kwa Mola.    


(Picha kwa hisani ya Michuzi)


Monday, January 17, 2011

Maisha ya Mwanadamu Simulizi la Mola; BISEKO (RIP)




Ndg. Biseko - Master (kwenye nyota) akisikiliza kwa umakini taarifa ya Wagonjwa na Tiba katika kikao cha Asubuhi cha Watumishi wa Afya- Nyerere DDH kabla ya kuuliza maswali ambayo mara nyingi yaliibua  ama changamoto, udadisi na au utafutaji wa
utoaji Huduma bora zaidi za Afya kwa wagonjwa!
















Monday, January 3, 2011

UVUMILIVU NA SUBIRA CHANGAMOTO TOKA KWA BABA



KUMBUKUMBU (4) YA MZEE A. MUTARAGARA CHIRANGI

Pamoja na Mwanafalsafa Friesrich Nietzsche (1844 - 1900) kuona na kusema kweli kwamba, kuwa na subira au uvumilivu ni ngumu sana, hata kwa Washairi Wazamivu kushindwa kuzuia hasira zao kutoa  dhamira ya ushairi wao au kwamba shauku haitasubiri!,

 Tulimsikia na kumwona baba Mzee Mutaragara Chirangi (RIP), akionyesha uvumilivu katika anga za Siasa kwa hali isiyotegemewa.



Ni siku nyingine tena leo, ikiwa imetimia takribani miaka minne tangu atutoke duniani, tunaendelea kupata kumbukizi la changamoto toka maisha ya  huyu mzee wetu.

Katika anga za ki- Siasa hususan baada ya chaguzi, uwezo wa Binadamu wengi kuweza kuvumilia au kunyenyekea au kuonyesha subira au kujizuia kusema au kufanya jambo ambalo halina tija wala maendeleo ya mwanadamu kwa leo na kesho, ni mdogo sana.

Dhamira ya uvumilivu aliyoitangaza mzee Chirangi kwa vitendo, kamwe haikumaanisha kushindwa kudai haki au kupigia debe maisha ya kukosa misimamo, la hasha;  bali uwezo wa kutulia baada ya uchaguzi na kuchambua hali halisi na kuchukua hatua muafaka pasi jaziba,  husuda wala chuki zisizo na maana.

Wenye kumbukumbu, wanaelewa ni mara ngapi mzee huyu aliwahi kugombea nafasi mbalimbali katika njanja kadha wa kadha, akashindwa na miitikio yake ilikuwaje na hata pia ilipotokea akashinda alisema na kufanya nini kwa waliokuwa washindani au hata wapinzani wake.

Hebu tusome sehemu tu ya moja ya Hotuba zake aliyoitoa Agosti 1987,baada ya kutoa huduma kwa mfululizo wa miaka 15 kama Mwenyekiti wa CCM  Musoma mjini. Nanukuu:

Kama ambavyo nimekuwa nikisema na kutenda, ieleweke wazi kuwa kiongozi achaguliwaye kwa kutoa fedha, ataongoza kwa kuchukua fedha, vilevile achaguliwaye kwa kufuata ukabila, atasimamia kabila, naye yule achaguliwaye kwa kampeni moto toka juu huenda akaondolewa kwa kampeni baridi kutoka chini.
Aidha, ni kitendo cha kutokukomaa kisiasa, kujenga chuki na hasira kwa mtu yeyote eti kwa sababu ya kutokupigia kura, kukushinda kwenye uchaguzi au kuazimia kugombea nafasi uliyodhani umetengewa wewe pekeke”.







Japo umelala baba, sauti  na maisha yako yataendelea kutufunza milele na milele.
Kwa kila jambo kuna majira yake.....!


Musuto wa – Chirangi
Kny. Familia Yote
03/01/2011