Friday, September 21, 2012

Uko wapi usalama wa waandishi wa habari wawapo kazini



Uko wapi usalama wa waandishi wa habari wawapo kazini
Hili lilikuwa swali la Kipindi cha ITV cha Malumbano ya Hoja la tarehe 20/09/2012

Nami naona maeneo manne ya muhimu kwa usalama wa Mwanahabari: 

1.    Mwanahabari mwenyewe:  NO STORY IS WORTH YOUR LIFE." So pull out before it's too late.   Awe na stadi za msingi za kujilinda inapobidi, asijisababishie hatari (kuripoti uongo, kuchafua wengine kwa uongo au mambo yasiyo na tija katika jamii) na awe na kitambulisho kinachoonekana(inapostahili), na  vifaa vya kujilinda (protective gears) awapo kwenye eneo la vurugu / hatari.      
               
2.    Mwajiri / Mhariri mwandamizi: lazima afanye utafiti wa eneo la kutolea habari (risk assessment) kabla hajamtuma mwandishi kama ni mahala pa hatari na awe na mawasiliano ya moja kwa moja na utayari kumwokoa endapo kuna shida. Wanahabari wote lazima wawe mikataba mizuri ya ajira, bima ya afya na maisha. Majukwaa na vyama vya Waandishi wa habari pia viko katika kundi hili kuhakikisha kuwa maisha ya Mwanahabari hayako hatarini na kwamba anafanya kazi yake kwa kufuata maadili ya kazi yake na kwa uhuru 

3.    Mihimili ya dola (Bunge, Serikali na Mahakama): Vyote vinapaswa kumlinda Mwanahabari kama ilivyo kwa raia wote kwa Bunge kutunga sheria bora, Serikali kusimamia sheria, kanuni na taratibu na mahakama kutafsiri sheria na kutoa haki. Polisi ni chombo cha dola hivyo kinapaswa kutimiza wajibu wake kwa haki na kuwafikisha wakosaji mbele ya haki bila kutumia nguvu zisizo za lazima.

4.    Raia wote: kwa kuthamini mchango wa mwanahabari popote na kuwapa ushirikiano

Nawapongeza ITV kwa kuanzisha mijadala kama hii kwa uwazi.

Nawasilisha;


Wa- Chirangi

No comments: