“…Why should my face not look sad when the city where my fathers are buried lies in ruins, and its gates have been destroyed by fire?" Nehemiah 2:3
MISINGI 10 ALIZOTUMIA MWANA DIASPORA SHUJAA
1. Kuwa na mawasiliano endelevu na nyumbani kujua si tu habari za kifamilia lakini pia maisha ya jamii na maendeleo yao kwa ujumla.
2. Kuwa na mzigo na matatizo yaliyoko nyumbani.
3. Kumshirikisha Mola katika mipango na mafanikio yetu.
4. Kutumia fursa na rasilimali tulizo nazo kwa ajili ya maendeleo ya jamii yetu
5. Kufanya tathinini za kisayansi za matatizo / mahitaji yetu halisi na kuweka mipango kazi na mikakati.
6. Kuhamasisha wengine na kugawana majukumu ikiwezekana kwa kujali vipaji / uzoefu / uwezo wetu.
7. Kushiriana pamoja kutekeleza mipango kazi.
8. Kutokuyumbishwa wala kukatishwa tamaa na wanaotubeza na au wanaotaka kutuondoa katika maono na mwelekeo wetu wa ki-maendeleo.
9. Kuonyesha ushujaa, kujilinda na ikibidi kupambana na wale wanaotaka vita na sisi.
10. Kusimamia haki, maadili na kuwajali wahitaji zaidi.
Kanuni hizi nimezinyambulisha nilipomkumbuka Kiongozi - shujaa mmoja katika Agano la kale, aliyeitwa Nehemia.
TAFADHALI KAMA HUJAWAHI SOMA AU KUTAFAKARI KWA UNDANI KITABU CHA NEHEMIA WAKATI NDIO SASA!
N.B Hata katika misaafu mingine kama Koran na hali kadhalika Hadith kuna mashujaa na wanamapinduzi wengi tu kama Nehemia.
Kwa kifupi tu ili kukupa hamu ya kusoma,
Nehemia alikuwa mshika kombe (the Cup- bearer) wa Mfalme wa Uajemi. Pamoja na kuwa katika maisha mazuri huko ughaibuni na katika hiyo kazi ya watu wachache sana katika ‘special branch’, katika kuwasiliana kwake na nyumbani, alipata habari kuwa kuta za Yerusalemu & malango yake vimebomolewa na kuchomwa moto.
Alibeba mzigo wa taabu zilizokuwa zinawakabili watu wa nyumbani Jerusalem, akahuzunika na kuomboleza sana.
Akamwomba Mola juu ya jambo hilo
Akatumia nafasi yake kumwendea Mfalme ambaye alimpa ruhusa na kumpa usalamana pia vitendea kazi vya kuanzia kazi ya ujenzi. (Sisi tunatumiaje vipawa na nafasi tulizo nazo kuendeleza jamii zetu?)
Alipofika kabla ya kuanza kazi alifanya tathmini ya kiwango cha uharibifu na kazi iliyotakiwa kufanywa na kupanga kazi.
Akahamasisha wenzake na kuwaambia kuwa tujenge pamoja, kazi iligawanywa vyema kufuata uzoefu/ uwezo. Mfano Makuhani walipewa kushughulia mlango waliouzoea na kuufahamu – mlango wa kondoo!
Watu walishirikiana wakachapa kazi mchana na usiku
Kuliibuka akina Sanbalati, Tobian na wenzao wakawabeza na kutaka kuwaondoa kazini, lakini Nehemia alisisitiza kuwa hawezi kuacha kazi.
Maadui walipopanga njama, ulinzi mkali uliwekwa na wakapambana nao. (Ni aibu sisi leo tunakatishwa tamaa wala hatupambani na maadui wetu katika maendeleo!)
Nehemia aliwasimamia haki kama kuwasaidia maskini n.k na pia akawawajibisha wakiukaji ili kulinda maadili yaliyokubalika.
Hitimisho:
Yawezekana tukawa na maisha bora zaidi popote tulipo nje ya mji au nchi, inatubidi kubeba mzigo na kuhuzunika na hali yoyote mbaya (kama ipo) katika jamii zetu. Mbele ya Viongozi wetu au Mashirika yenye uwezo au yeyote mwenye uwezo wa kutusaidia kutatua tatizo lililopo, tunapaswa kusema kuwa,
“Tutakosaje kuwa na huzuni wakati mji/ nchi ya baba zetu na mama zetu ina hali isiyoridhisha?”
Halafu tufanye kweli kwa tuchukuwa hatua 10 za kuleta maendeleo kama kiongozi wa mfano Nehemia alivyofanya.
Verbal Diarrhoea Dehydrates Human Dignity. Chirangi (2000).
No comments:
Post a Comment