Wednesday, November 17, 2010

A New Health Centre in Musoma


Tumetangaziwa na Uongozi husika kuwa, Kituo cha Afya kipya kwa jina Bethsaida Health Centre, kilichoko katika kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma  kinaanza kutoa huduma za Afya kwa Wananchi kuanzia 17/11/2010.

Natoa wito kwa:
  • Watumishi wa Kituo hiki kipya,  kuwa wajitahidi kutoa huduma bora isiyo aghali huku wakitii taratibu ziongozazo na maadili ya Taaluma zao kwa moyo, nguvu na akili zao zote.

  •  Uongozi wa Kituo, kutumia kanuni za Menejiment bora na Mawasiliano yenye ufanisi  huku wakijali Watumishi wao na kutathmini shughuli kila wakati ili kuboresha kiwango na ubora wa huduma kwa Wateja.

  • Manispaa yetu  na Wananchi kwa ujumla kuunga mkono juhudi hizi kwa kukubali kuwa na makubaliano ya mkataba wa utoaji huduma kwa ushirikiano wa Serikali & Sekta Binafsi  (Public - Private Partnership)  ili kuwezesha kupunguza gharama za uendeshaji na hivyo gharama za matibabu kwa Wananchi.

Sote tunamshukuru Mungu na wote waliowezesha huduma hii kuwepo.  Aidha tunamkumbuka Mzee wetu Mutaragara (RIP), mtu wa watu ambaye eneo na nyumba yake milki ndipo kituo hiki kimejengwa.


********************************************


1 comment:

msomian said...

mzee wa viwango tunashukuru kwa hii huduma endelea kuisimamia ili kusudi lake litimie kutusaidia wananchi maana huduma za afya si za viwango hapa na hazipatikani kwa urahisi.