B
Azikwa Musoma, tarehe 27/072011.
BURIANI ASK. MSTAAFU SALMON SARIGE BUTENGÉ
Uwepo wa utulivu mahala hapa ni heshima, tafakuri na kujihoji wakati tunapata rejea ya safari ya maisha ya Mtenda-kazi wa Bwana, Ask. Salmon Sarige Butengé japo kwa dakika moja.
Ewe kifo, unaweza kuitenga miili yetu lakini kamwe huwezi kuzitenga roho zetu, huwezi kuifuta miguso wala kumbukumbu za maisha ya Wapendwa wetu.
U wapi mauti na machungu yako? Hatukuongelei tena kwa kuwa umaarufu wako ulishafunikwa na Ufufuo na Tumaini alilotuachia Bwana wetu Yesu Kristo.
Kama hamasa toka kwa Bibi Mahalia Jackson ilivyomgusa Mch. Martin Luther King, Jnr, na hatimaye kuteremsha mistari ya karne “Nina njozi” (I have a dream), ndivyo tulivyoweza kushuhudia hamasa ya kishujaa, isiyomungúnya maneno ya mama yetu, Bibi Ask. Lois Sarige Butengé akinena,
"Yaika! wa Butengé, yaika!", katika kadamnasi hususan wakati wa Makambi pindi Mchungaji / Askofu Butengé alipokuwa akitema cheche za injili mathalani juu ya somo la Mtenda-kazi wa Bwana au Maji yaliyo hai n.k, huko Mugumu, Bumangi, Majita, Mugango, Musoma, Nyabange, Shirati, Mwanza, Dar es salaam na kwingineko.
Ee Mola, kama huko Mbinguni pangehitajika Mkutano wa Kiroho, tusingesita kutamka kuwa Mjoli wako Salmon Sarige uliyemtwaa ni mmojawapo wa Rasilimali-Binadamu mwenye taranta husika.
Bwana umetwaa, Jina lako linaendelea kubarikiwa na bila shaka mwangwi wa sauti ya mama Lois, sasa imepokelewa na malaika wakiimba,
"Gendelela okwaika wa Buteng’e, gendelela okwaika! "
Wana Familia, Jamaa, Marafiki na Wana – KMT kwa ujumla poleni sana kwa msiba huu.
Ni sisi
Judy, Marja & Musuto wa- Chirangi.
Judy, Marja & Musuto wa- Chirangi.
Utrecht, the Netherlands
26 Julai, 2011