Friday, October 10, 2008

BURIANI DR. MAGAI KAARE


DR MAGAI - mtu wa kazi mjoli wa watu


Kama vile ndege waendeleavyo kuimba wakati wa mvua ya masika, nasi tunaendelea kusifu maisha ya mfano ya marehemu, Kiongozi Mjoli wa watu Dr. Magai Kaare wakati huu wa Msiba.

Kama vile maua yanavyonyauka na kuacha mbegu, sote tulio bahatika kuendelea kupumua pumzi ya uhai tuendeleze mema aliyoyaanzisha ikiwa ni pamoja na kumtunza mkewe Lega na watoto wao Dorka & Joyce. Aidha tunapaswa kuunga mkono kwa vitendo mawazo na mapendekezo ya


mabadiliko ya sera na mikakati tokana na Tafiti za kisayansi za Mwanataaluma huyu mahiri hususani katika kudhibiti milipuko ya magonjwa ya wanyama pori na wa kufugwa yanayoathiri siha za wanyama na wanadamu katika nchi zinazoendelea.

Magai, tulikufahamu si tu kama rafiki wa karibu bali mwanadamu ulieamini kuwa ni vema kuwasha mshumaa kuliko kulaani giza katika changamoto mbalimbali za ulimwengu wa sasa!

Machozi yetu ya uchungu ni mbadala wa maneno yananayobaki bila kusemwa na matendo tuliyoshindwa kuyatekeleza kutokana na uwezo wetu wa kibinadamu.

Kwa kila jambo kuna majira yake

Tunatoa pole kwa Wana-familia, Jamaa, Marafiki, Watumishi na Watafiti wezake chini ya mradi wa kimataifa wa Infectious Diseases of East African Livestock (IDEAL), Uingereza.

Tunawasilisha leo wakati wa Mazishi huko Musoma- 09/10/2008


wa- Chirangi
___________________________________


















Lega, Dorka & Joyce

2 comments:

Anonymous said...

siku zote utakumbukwa!RIP

Anonymous said...

Poleni sana kwa msiba huu mkubwa.
Mola amfariji mkewe na watoto wao.