Friday, May 29, 2009

PAZIA LA HEKALU LIKAPASUKA

Somo: Marko 15: 38
“Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini”
Kufa kwa Yesu kulituletea njia mpya ya upatanisho na Mungu na pia baina ya Wanadamu.
Kupasuka kwa pazia kuna maanisha:

1. Uwepo wa fursa sawa katika njia ya wokovu.
Waebrania 10 :19 “Basi, ndugu kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo hai, ipitayo katika pazia , yaani mwili wake ”.
Kifo cha Yesu Kristo kimeleta njia mpya ya wokovu iliyo karibu na Mwanadamu (Pazia liliwaweka watu mbali na Mungu). Waefeso 2:13 “lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu ya Yesu kristo”
Mwendelezo wa ‘UPAZIA’ umeleta dhana potofu ya maisha ya ‘the sacred & the secular Citizenship’.

2. Uwepo wa umoja wa wanadamu na uvunjwaji wa matabaka yanayolenga kubinya haki na fursa.
Kati ya Watu wa Mataifa & Wayahudi (Watakatifu); Watwana na Watumwa; ‘Weusi na Weupe’ ; Wanawake na Wanaume; Wenyeji na Wageni; Waleta dini na Waletewa dini, Watiwa mikono na Walei; Wazee na Watoto; Wasomi na wasio Wasomi; Wataalamu na wasio na Utaalamu; Matajiri na Maskini, Viongozi & wanaoongozwa, Wagonjwa na ‘Wenye afya’ n.k
Waefeso 2: 14 “Kwa maana yeye ndiye amani yetu , aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja, akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga”
Hitimisho:
Waandishi wa Agano jipya wanapoelezea kusulubiwa na kufufuka kwa Yesu hawakusudii kutuonesha vitisho na ukatili wa kimwili katika kifo chake wala rushwa, hukumu batiri na uongo uliosambaa bali umaana wake ikiwa ni mpango kamili wa Mungu katika kumkomboa wanadamu kwa kumpa fursa na upatanisho (1Petro2:24). Tutumie neema hii kwa kushiriana kwa ajili ya kuboresha huduma

1 comment:

censor lee said...

well summarized meaning of Easter- wa Chirangi