Uko wapi usalama wa
waandishi wa habari wawapo kazini
Hili lilikuwa swali la Kipindi cha ITV cha Malumbano ya Hoja la tarehe 20/09/2012
Nami naona maeneo manne ya muhimu kwa usalama wa Mwanahabari:
1. Mwanahabari
mwenyewe: NO STORY IS WORTH YOUR LIFE." So pull out before it's too
late. Awe na stadi za msingi za kujilinda inapobidi,
asijisababishie hatari (kuripoti uongo, kuchafua wengine kwa uongo au mambo
yasiyo na tija katika jamii) na awe na kitambulisho
kinachoonekana(inapostahili), na vifaa
vya kujilinda (protective gears) awapo kwenye eneo la vurugu / hatari.
2. Mwajiri / Mhariri mwandamizi: lazima
afanye utafiti wa eneo la kutolea habari (risk assessment) kabla hajamtuma mwandishi kama ni
mahala pa hatari na awe na mawasiliano ya moja kwa moja na utayari kumwokoa
endapo kuna shida. Wanahabari wote lazima wawe mikataba mizuri ya ajira, bima ya afya na maisha. Majukwaa na vyama vya Waandishi wa habari pia viko katika kundi hili kuhakikisha kuwa maisha ya Mwanahabari hayako hatarini na kwamba anafanya kazi yake kwa kufuata maadili ya kazi yake na kwa uhuru
3. Mihimili ya dola (Bunge, Serikali na
Mahakama): Vyote vinapaswa kumlinda Mwanahabari kama ilivyo kwa raia wote kwa Bunge
kutunga sheria bora, Serikali kusimamia sheria, kanuni na taratibu na mahakama
kutafsiri sheria na kutoa haki. Polisi ni chombo cha dola hivyo kinapaswa
kutimiza wajibu wake kwa haki na kuwafikisha wakosaji mbele ya haki bila kutumia nguvu zisizo za lazima.
4. Raia
wote: kwa kuthamini mchango wa mwanahabari popote na kuwapa ushirikiano
Nawapongeza ITV kwa kuanzisha mijadala kama hii kwa uwazi.
Nawasilisha;
Wa- Chirangi