KWA HESHIMA YA MZEE MUTARAGARA CHIRANGI ( Nyarutangwe - Omwana wa Nyamurugwa wa Kafwenyi). ALISUKUMWA NA DHANA YA KUTENDA HAKI NA KUISHI KWA 'STD' INAYORIDHISHA. ALIONGEA JUU YA HAKI, AKATENDA HAKI KI-STD, AKAITWA MZEE WA STD-MTETEZI WA HAKI. NJOO TUSHAURIANE JUU YA KUBORESHA MAISHA YETU ILI TUISHI KATIKA HAKI NA KWA STD INAYORIDHISHA
Friday, August 31, 2012
Udanganyifu katika Mitihani - Swali la kipima joto
Jawabu la kukabili udanganyifu katika mitihani ya shule za msingi liko katika kuhakikisha kuwa tunakuwa na mfumo endelevu wa utoaji na usimamizi wa elimu bora na tathmini yake kuanzia Wizarani hasi Shuleni (a sustainable and effective quality assurance system of education). Mfumo huu lazima uangalie inputs zote yaani rasilimali-wanadamu (Waalimu, Watumishi wengine & Wanafunzi), sera, mitaala, miundombinu, vitendea kazi na pia michakato (processes) na bila kusahau stadi katika usimamizi wa mitihani (examination administration).
wa - Chirangi
BURIANI MAMA BERTHA KIFUTU
Kwa huzuni, tunapotafakari kututoka kwa ghafla kwa mpendwa Mama yetu Bertha Kifutu, tunaendelea kukumbushwa kuwa kifo si kutoweka kwa mwanga wake, bali kuzimwa kwa taa yake wakati wa mapambazuko baada ya kukamilisha safari ya maisha yake hapa duniani.
Ingawa Mwandishi, Hans Christian Andersen, alitukumbusha kuwa, maisha ya Mwanadamu ni hadithi isimuliwayo kwa ukamilifu na Mola, turuhusuni
nasi tusimulie japo kwa kudodosa rejea ya maisha ya huyu Mama yetu japo kwa aya
moja, kama Mithali ya Mfalme Solomoni Mwana wa Daudi inavyosimulia;
Kwamba, Mwanamke mwema, kwa mikono yake, hufanya
kazi zake kwa nguvu na Wanawe humwita Mbarikiwa, pia huamka kungali giza (asubuhi
na mapema), kuangalia mambo ya nyumbani kwake, wala hali chakula cha uvivu; hivi
ndivyo ilivyokuwa pia kwa huyu Mama yetu, Sengi Nyamambala wa Makanya
hadi mauti ilipomkuta asubuhi na mapema (katondo-
tondo muruguru) akiwa mfano wa Mama aangaliae mambo ya nyumbani kwake na kutunza
familia!
Hakika, ingawa kifo kinatuondolea wapendwa wetu,
kamwe hakiwezi kutuondolea fikra na
matendo yao ya kishujaa. Aidha, kwa vile huacha katika kumbukumbu zetu, alama za
upendo zisizofutika kwa jinsi walivyoshirikiana nasi, basi tumuombe ndg. Sira, Kiongozi
wa iliyokuwa kwaya yake (Imani - Choir), Kanisa na Jamii kwa ujumla,
tuendeleze hamasa na jitihada za mpendwa wetu katika kuishi maisha ya kumtukuza Mungu wetu kwa furaha.
Swali kuu la kujiuliza; je, sisi tumempa Mungu kipi
cha ziada kuturuhusu kuingia katika kumbukumbu za Sensa ya Taifa ya Watu na
Makazi leo tarehe 26/08/2012, ilhali makucha ya mauti hayakutoa nafasi hata ya siku
mbili tu wala kwa familia ya mpendwa wetu kuweza hata kusikiliza tamko lake au
kuagana naye?
Katika huzuni twaomboleza, katika
huruma twawafariji wafiwa, katika tafakuri twajihoji juu ya maisha na uhai wetu-
swali lisilojibiwa hata na Wana-Baijirontolojia (Biogerontoligists) wazamivu wanaotafiti
namna ya kurefusha miaka ya kuishi uzeeni!
Pamoja
nanyi katika maombolezo,
Judy,
Marja & Musuto wa Mutaragara wa Chirangi
Subscribe to:
Posts (Atom)