KWA HESHIMA YA MZEE MUTARAGARA CHIRANGI ( Nyarutangwe - Omwana wa Nyamurugwa wa Kafwenyi). ALISUKUMWA NA DHANA YA KUTENDA HAKI NA KUISHI KWA 'STD' INAYORIDHISHA. ALIONGEA JUU YA HAKI, AKATENDA HAKI KI-STD, AKAITWA MZEE WA STD-MTETEZI WA HAKI. NJOO TUSHAURIANE JUU YA KUBORESHA MAISHA YETU ILI TUISHI KATIKA HAKI NA KWA STD INAYORIDHISHA
Saturday, August 24, 2024
Saturday, January 1, 2022
Saturday, December 30, 2017
Asanteni Sana WanaCCM 2017
Wanachama wa CCM; Rafiki na ndugu zangu;
Asanteni sana kwa kunitia moyo na kunifanya kuwa Mgombea Uwenyekiti CCM Mkoani Mara.
"Mpira wangu waweza kuwa umegonga nguzo ya goli; lakini bado upo uwanjani ; bado upo mchezoni"
Ada ya mja hunena Muungwana ni kitendo. Kwa kila jambo na majira yake. Tutakiane Kheri katika mwaka mpya wa 1918.
Labels:
CCM,
chirangi,
Musoma Mara,
Musuto,
mutaragara,
Uchaguzi Mkuu
Tuesday, March 22, 2016
REST IN PEACE - COMRADE SOSPETER KONGOLA KARAMBA
BURIANI KAMARADE SOSPETER KONGOLA WA KARAMBA
Kwa
mara nyingine tena, kauli isiyobadilika wala kuulizwa ya Mola wetu pale
Bustanini Edeni, akinena “….hakika mtakufa” imetimia: Tarehe 18/03/1016, mauti imezuru katika
familia ya Karamba!
Kwa
butwaa na huzuni mkubwa, tulipokea taarifa hiyo iliyobeba simanzi tokana na
kifo cha Kijana Sospter Kongola akiwa
katika matibabu huko Dar es salaam.
Ewe Mauti ya Mwili
kamwe, hutaweza kutuondolea kumbukumbu ya ushirika usio mipaka na huduma
njema zenye umilisi na adala ya mtu wa watu, mdogo wetu Kongola.
Tunakiri kuwa kifo huleta simanzi, lakini imani
husababisha fikra tunduizi za maisha baada ya maisha ya hapa duniani. Pale
ambapo, tunasema ni mwisho wa maisha ya kiwavi, hakika ni mwanzo wa maisha ya
kipepeo! Japo amekufa, mdogo wetu ameanza maisha mapya!
Ewe kifo, waweza
kusababisha mtanziko; tena una uwezo wa kuitenga miili yetu lakini kamwe huwezi
kuzitenga roho zetu; huwezi kuzifuta hisia zetu, kumbukumbu za maisha wala picha isiyofutika ya
tabasamu la Kongola lililoashiria ushirika wake katika jamii.
Tunamkumbuka kwa mengi ya kutufunza sisi ambao bado
tunaendelea kujaliwa nafasi ya kuishi hapa duniani. Sosy
atakumbukwa kwa ucheshi na kujenga mahusiano na watu wengi huku akiwapa misaada mbalimabli iliyokuwa
ndani ya uwezo wake.
Tunakiri kuwa: “KIFO HUACHA MAUMIVU YA MOYO, HAKUNA AWEZAYE
KUYATIBU,
BALI UPENDO HUACHA KUMBUKUMBU, HAKUNA AWEZAYE
KUIIBA”. KOMREDI SOSY KONGOLA, KATIKA KUSANYIKO HILI LENYE SIMANZI, UPENDO
WETU KWAKO UMETUACHIA KUMBUKUMBU
ISIYOIBIWA AMBAPO TUNAENDELEA KUKUPIGIA SALUTI TUKIENZI CHAPA ULIZOTUACHIA KATIKA SAFARI YA MAISHA YAKO
HAPA DUNIANI.
PENGINE WENGINE
WATAELEZA MENGINE YANAYOJIKITA KATIKA MAPUNGUFU YAKO KAMA BINADAMU AMBAYO HATA
WAO WANAYO; SISI TUTAENDELEA KUELEZA NA KUJIFUNZA NA KUYATUNUKU MAISHA YAKO YA:-
Ø UCHESHI
NA UTANASHATI
ULIOTUKUKA MAHALA POPOTE, KILA
WAKATI ,
Ø URAFIKI NA USHIRIKA MWANANA KWA WATU WENGI PASIPO
MIPAKA ISIYO NA TIJA,
Ø UTUMISHI WAKO HODARI KAMA
MFANYAKAZI KATIKA IDARA YA AFYA NA
USTAWI WA JAMII ULIYEAJIBIKA KWA MAADILI
YA UTUMISHI WAKO,
Ø USHIRIKI WAKO KWA VITENDO KATIKA SHUGHULI ANUAWI ZA SIASA, MAENDELEO YA
KIJAMII NA KIUCHUMI.
Si maandishi wala machozi yetu, yanayoweza kuonyesha kwa
ukamilifu huzuni tuliyo nayo moyoni
mwetu kwa kuachwa na mpendwa wetu. Nawasihi tumuenzi Kongola kwa kuiga yale
mema aliyoyatenda katika jamii.
Wana
Familia, Jamaa, Marafiki,Wana – KMT, Wana CCM na wafiwa wote kwa ujumla poleni sana
kwa msiba huu.
Faraja kuu na mioyo ya subira iwe nasi
sote toka kwa Rabuka wetu hata katika mwamba huu tusioweza kuupanda kama Zaburi
61:2 ituelekezavyo:
“Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia
moyo, uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.”
Tunawapa
pole wafiwa wote kwa msiba huu mkubwa.
Buriani Sosy, Buriani Komredi Kongola.
Dkt. Musuto wa Mutaragara wa Chirangi
Mmoja wa Rafiki Wengi wa Kongola.
Friday, November 6, 2015
KILA LA KHERI, SOTE TUSHIRIKIANE KUFANYA KAZI TU!
Baada ya kula viapo stahiki, mbele ya Jaji Mkuu;tunamtakia
Rais na Amiri Jeshi Mkuu wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kila la kheri katika majukumu hayo makubwa na ya juu nchini kwetu.
Aidha sote tunabaki na wito wa kuweka kando tofauti zetu na kudumisha umoja wa kitaifa huku tukifanya kazi kwa bidii na uadilifu kwa ajili ya maendeleo yetu na Taifa letu kwa ujumla.
Thursday, October 29, 2015
Hongera Prof. Dkt. S. Muhongo - Mbunge Mteule
Kwa uelewa na mapenzi ya wananchi wa Jimbo lake wakizingatia Kauli Mbinu yake:
'TUKUZE UCHUMI ;TUONDOE UMASKINI PAMOJA'
Wananchi wameongea kupitia sanduku la kura.
Tunamtakia kila la kheri katika uwakilishi wa Jimbo na katika kulitumikia Taifa kwa ujumla.
Tuna imani naye katika uwajibikaji wa kweli katika kukuza uchumi kwa maendeleo ya Watanzania wote.
Shukrani za kipekee, zimfikie Mkewe, Mama yetu, Bibi Bertha Muhongo (Msc, MBA), Timu nzima ya Kampeni na wote walioshiriki katika kufanikisha ushindi huu, hususan Wapiga Kura - Wananchi wa Musoma Vijijini.
Saturday, October 24, 2015
SHUKRANI KWA WANANCHI: OMWAKA GWO OBHWATASYO NA IMPOKOCHOLE.
Kama ambavyo niliendelea kufanya toka tarehe 01/08/2015; naendelea kuwashukuru kupitia blogu yangu watu wote walioniunga mkono na hata ambao hawakuniunga mkono kwa namna moja au nyingine katika Kura za Maoni katika nafasi Ubunge Jimbo la Musoma Mjini.
Waweza sikiliza na kudadavua zaidi kwa kujikumbusha vionjo vya 'Omwaka gwo Obhwatasyo na Impokochole' hapa:
Maisha yanaendelea, hata baada ya Uchaguzi!
Tanzania Tubaki kuwa Kisiwa cha Amani!
wa- Chirangi, PhD
Subscribe to:
Posts (Atom)