Thursday, November 26, 2009

VETERANS

SOCCER VETERANS

Mara nyingi, Ma- 'Veterans' hutumika kwa wastaafu au watu waliotumika muda mrefu katika Majeshi. Hata hivyo ni bayana kuwa jina hilo pia tunaweza kuliazima na kulitumia kuwaenzi watu waliotumikia fani za michezo.
Katika historia ya Mpira wa Miguu Tanzania, mkoa wa Mara bado haujatukuka sana ingawa katika michezo mingine kuna Timu kama vile Buhemba JKT Handball Team na Magereza Mara - Netball Team wamewahi kuutoa Mkoa Mara kimasomaso.

Aidha kuna Wachezaji na Wasanii mmoja mmoja ambao ama walitokea Mkoani Mara au wana nasaba ya watu wa Mkoani Mara  pia walionekana nyota katika kushiriki michezo na sanaa mbalimbali nchini na nje ya nchi. Hawa ni kama vile Mujaya Suleiman Nyambui (Athletic), Mahesa (Basketball); Fehadah Faru (Netball); Ali Mchumila, Lucas Jamberi, Nico Bambaga, Bite John, Castor Mumbara  (Soccer); Judith Wambura, Nyangómboli , Maringo Omwichukuru wa Kabondo-imbwa ya Salehe  (Musicians); Sele Kum-cha (Karate)- na wengine wengi ambao kamwe sitaweza kuwaorodhesha wote.

Hata hivyo tunawakumbuka na kuwaenzi wachezaji wote wakongwe waliowahi kucheza katika vilabu maarufu  vya soka huko Mara kama vile timu ya Kazi, Usagishaji, Maji, RTC,Tanesco, Mutex, Posta & Simu, Mugango, Musoma Shooting, Tarime, Seronela, Amani  na Timu machachari ya  muungano - Mara Stars.
Hapo juu ni picha ya pamoja ya baadhi ya Maveteran hao waliowahi kuchezea vilabu hivyo wakiwa katika uwanja wa Posta - Musoma (2008).

No comments: