Uchaguzi umekwisha, Rais J.Kikwete ameshaapishwa tayari kuunda na kuongoza Serikali kwa kipindi cha miaka 5.
Pamoja na matukio ya hapa na pale, Mimi na familia yangu tunawapongeza Watanzania wote kwa jinsi mlivyoendeleza amani wakati wote wa Kampeni hadi kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu.
Tunamwombea Rais, Makamu wake Mh. M.G.Bilal, Mawaziri na Viongozi Wengine wote wa Mihimili ya Taifa katika ngazi zote, afya njema, maono na uongozi wenye ufanisi katika Nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.
Niliguswa sana na kauli ya "Tusigombee Fito", hivyo nami natoa mwendelezo wa wito huo kuwa :
'Shime Watanzania wote, pasi kujali tofauti zetu za ki-itikadi na vyama vyetu vya siasa, tutafute fito za kutosha na tusaidiane ili kujenga nyumba yetu kwa ushirikiano.'
Tanzania itajengwa na Watanzania Wenyewe.
Mungu ibariki Tanzania.
Wakatabhau,
Judy, Marja & Musuto wa- Chirangi
**********************************************************
**********************************************************
1 comment:
wa- Chirangi wewe huwa una uwezo mkubwa ktk kujenga hoja, kuandika na hata kuongea kwa ufasaha ukaeleweka. Unafaa sana ndg. na hiki ni kipawa chako toka tukiwa wote shuleni (LJS) nakumbuka hata ulivyokuwa mchambuzi.
Niliona blog yako huko kwenye twitter, nikakutembelea.
LJS Alumnus.
Post a Comment