Friday, November 6, 2015

KILA LA KHERI, SOTE TUSHIRIKIANE KUFANYA KAZI TU!

Baada ya kula viapo stahiki, mbele ya Jaji Mkuu;tunamtakia 
Rais na Amiri Jeshi Mkuu wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.  John Pombe Joseph Magufuli kila la kheri katika majukumu hayo makubwa na ya juu nchini kwetu. 
Aidha sote tunabaki na wito wa kuweka kando tofauti zetu na kudumisha umoja wa kitaifa huku tukifanya kazi kwa bidii na uadilifu kwa ajili ya maendeleo yetu na Taifa letu kwa ujumla.

1 comment:

Anonymous said...

Asante baba sasa ni kazi tu! Mungu ambariki na kumpa afya na hekima atuongoze sawasawa na ahadi zake na pia ilani.