Friday, July 4, 2008

KAZI INAENDELEA !

PROBLEM STATEMENT


Majority of Mara residents like those of other developing countries are characterized with poor health status, which is also a causal-effect element of the overall poverty.
Among different causative factors, poor and inadequate health services are major factors in the region. This is due to mainly a combination of insufficient human resources, inadequate medical supplies & equipment and too much workload to few available Health Facilities to respond to diverse individual and community health related needs.


BELOW ARE PICTURES OF THE PRESENT CONTINUED WORK OF THE PROPOSED BETHSAIDA HEALTH FACILITY TO CONTRIBUTE IN RESPONDING TO THE IDENTIFIED PROBLEM.

































Thursday, May 1, 2008

"Friendship is a Single Soul Dwelling in Two Bodies"


Katika uzinduzi rasmi wa Kanda ya Afika ya ICSU.(http://www.icsu-africa.org/) September 2005,
Prof. Dr. Sospeter Muhongo wa Nyawayega
Mwanasayansi Mahiri na Mkurugenzi Mfawidhi wa ICSU-Kanda ya Afrika anadodosa Malengo ya Asasi hii ya Kimataifa, Hali ya Bara letu la Afrika na changamoto zinazotukabili.
(Ukipenda kupata muhtasari wa wasifu wa Mtanzania huyu kiongozi, bofya hapa: http://www.icsu-africa.org/icsuafricabios.htm#muhongo)
SEHEMU YA HOTUBA YAKE:


The Harsh Reality


About 40% of Sub-Saharan Africa (ca 250 million people) lives in absolute poverty








Akihitimisha hotuba hiyo ya ufunguzi, kiongozi huyu alimnukuu gwiji wa Falsafa na Mwanasayansi Aristotle (384KK -322KK) akisema,
"...friendship is a single soul dwelling in two bodies"

Hivyo basi sote kama Waafrika, ingawa tuna miili na nasaba anuwai ni vema tuwe marafiki kwa kunia mamoja kwa roho moja (with a single soul) ya kufanya Tafiti na kutumia Sayansi endelevu kwa ajili ya kuboresha Afya na Maisha yetu kwa ujumla!


































UKIRI WA CHIRANGI


Namuaminia[1] mnyama wa kisiasa mmoja, mzee wa busara aliyewaacha Wanasiasa, Wanahistoria na Wahabarishaji midomo wazi.

Nawatunuku pia Wapigania-Haki wengine kama vile Chifu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyiga, Martin Luther King, Julius Kambarage Nyerere, MamaTereza wa Calcutta, Mohandas Karamchand Gandhi, Bibi Aung San Suu Kyi wa Myanmar na wengine wote walio mifano kwetu.

Alizaliwa katika kijiji cha Qunu karibu na Umtata, Transkei. Rolihlahla akakua akiwasikiliza Wazee na akafundwa chini ya utamaduni asilia katika ufukwe wa mto Bashee zamani za Utawala wa Kiimla na Ubaguzi wa Rangi.
Katika harakati za Umkhonto we Sizwe na mchango wake dhidi ya utawala wa Makaburu, akachukiwa, akasingiziwa makosa ya kiuhaini, akashitakiwa na kufungwa kifungo cha maisha katika gereza la wafungwa sugu na lenye ulinzi wa hali ya juu kuliko yote.
Msimamo wake haukuyumbishwa na mpango wa kupewa takrima yenye ndoano, eti awekwe huru kinamna huku watu wake wanaendelea kutaabika.

Siku ya uhuru ikawadia, baada ya muda wa yapata miongo mitatu, akaachiwa huru akatoka katika harufu mbaya, mateso na upweke. Wananchi wakarejea katika demokrasia na haki; uchaguzi ukaitishwa.
Ndipo aliyekuwa mfungwa wa kisiasa alipoibuka mshindi kwa kura nyingi. Akaingia Ikulu akaketi katika kiti chaUraisi.
Akaongoza nchi, lakini kinyume na matarajio ya wengine, pia akawasamehe na kuwashirikisha Wabaya wake.
Pamoja na mamlaka aliyopata na kutunukiwa Mali, Ukazi wa Kimataifa, Shahada, Medali na Tuzo nyingi mbalimbali ikiwemo ya Amani ya Nobeli na hata jina lake kutambulisha barabara, tuzo na majumba katika Mabara yote Duniani bado aliendelea kuwa mtu wa watu, muungwana asiye na kiburi wala dharau.

Ninapenda kusimama katika Usawa, Haki, Demokrasia na Umoja uletao Ufanisi. Kwa vile Jitihadi haiondoi kudura, namwomba Mungu anisaidie niige mfano huu wa muasisi Nelson Mandela katika hali yangu nichaguapo viongozi, nigombeapo uongozi au nikabidhiwapo dhamana ya kuongoza.

Pasi kilinge nachukia hasilani maisha ya Ufalisayo yaliyokubuhu uzandiki na uburuzaji wa wanyonge.

Nakereketwa kutafuta, kujenga na au kurejesha amani popote nitakapokuwa.
Nina heshimu uongozi shirikishi wenye ushawishi mwanana unaojali utu wa mwana- adamu uliopitishwa katika tanuru la michakato ya kisayansi, maadili ya kitaaluma na utamaduni uliokubalika kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya mwanadamu.

Ada ya mja hunena muungwana ni kitendo Mungu nisaidie nitende sasa na hata milele.
Nyamuwanga nunsakile kajanende na kajanende!

[1] Tofauti na neno Namuamini, hapa ni kuwa na uhakika wa utendaji wa mtu na sio kumtukuza kama MUNGU

Sunday, March 30, 2008

wa- CHIRANGI AWAONDOLEA UVIVU WENYE VIBURI HASI

'KIBURI HASI NI KIKWAZO KIKUBWA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU NA MAENDELEO YAKE POPOTE'.

HII NI SEHEMU YA KWAZA YA HOTUBA YA MUSUTO wa- CHIRANGI AKIWAASI

WANA-SERENGETI JUU YA MADHARA YA KIBURI HASI.'

Monday, January 14, 2008

BETHSAIDA CENTRE FOR HEALTH AND DEVELOPMENT





UZIO WA 'THE HOUSE OF BETHSAIDA ' MAHALA AMBAPO PANATARAJIWA KUWA KITUO CHA AFYA KWA AJILI YA WANANCHI KATIKA MANISPAA YA MUSOMA SIKU ZA USONI.
HII NI HATUA MOJAWAPO YA KUMUENZI BABA MUTARAGARA CHIRANGI KWA KAZI YAKE YA HUDUMA KWA WANANCHI.
MAANDALIZI YATAKIWAYO YANAENDELEA KWA MUJIBU WA TARATIBU ZINAZOPASWA.
Imetolewa kwa hisani ya mpiga hizi picha P.Mamuya.

Thursday, January 3, 2008

KUMBUKUMBU ZA MWAKA MMOJA JUU YA MAISHA YA MZEE CHIRANGI




KIUMBE HADIMU AMBAYE JAPO AMEKUFA SAUTI YAKE NA MATENDO YAKE YANAENDELEA KUTOA CHANGAMOTO CHANYA KATIKA MAISHA YETU WANAMARA NA TAIFA ZIMA KWA UJUMLA.

Hakutoka katika familia maarufu wala hakuwa na mali nyingi na elimu yake ilikuwa tu ya wastani. Hata hivyo ukithubutu kunyambulisha mitizamo, misimamo na matendo yake waweza kubaini kuwa upatikanaji wa viumbe wenye matendo sanjari na kauli mbiu ya ‘HAKI HUINUA TAIFA’ ni adimu katika ulimwengu wa leo.

Siku kama ya leo, mwaka mmoja uliopita makucha ya kifo pasipo huruma wala taarifa yalituondolea pumzi ya uhai Mzee wetu


Amos Mutaragara Chirangi wa Muhongo wa Nyawayega wa Rihu- Omumbogo wa Kumusoma gwa Nyambita..

Marehemu mzee Chirangi aliyezaliwa mwaka 1932 huko Bushora Mwirengo Mugango, Mkoani Mara aliacha alama za kishujaa kama Kiongozi, Mzalendo na Muumini wa kuigwa katika kizazi hiki na vijavyo.

Familia ya Chirangi inawashukuru sana wananchi wote wa Mkoa wa Mara na kwingineko, Serikali yetu, Jumuiya zote za Kidini, CCM na Vyama vyote vya siasa, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Taasisi na Asasi mbalimbali za kijamii kwa Faraja, Misaada mbalimbali, Umoja na Mshikamano wao waliotuonyesha wakati wa msiba hadi huduma za mazishi za marehemu baba yetu Mutaragara Chirangi. Ni bayana kuwa hakuna chombo chochote cha habari wala mtunzi wala hifadhi ya makumbusho inayoweza kwa ukamilifu kutuhabarisha juu ya wasifu wa marehemu mzee Chirangi. Hata hivyo kweli isiyofichika huchomoza popote ikitukumbusha machache tu ya utu na utumishi wake kwa wanadamu. Kila mwaka familia yake itakuwa inaainisha dhamira moja kuu ambayo inaakisi moja ya sifa zake kama changamoto kwetu. Mwaka huu tunaanza na sifa yake ya UWEKAJI MIPANGO (Planning):-

Kila kitu chake alitaka kiwe kimeandaliwa barabara kwa wakati muafaka na kwa kiwango kinachoridhisha hivyo akaitwa ‘mzee wa Standard’. Ni mzee aliyepinga kwa vitendo uongozi na maisha ya uzima moto, ndiposa tulishuhudia hata akiwa amejiandalia Wosia kwa familia na kaburi lake mwenyewe sio kwa udhoofu wa afya yake bali kwa msingi wa kujiandaa na kutotaka kusababisha usumbufu wowote kwa jamii wakati anajua kuwa kauli ya Mungu pale Edeni kuwa ‘hakika mtakufa’ ni ya kweli na kwamba ilimuhusu pia hata na yeye.
Ni mzee aliyekuwa rafiki wa karibu wa nyenzo KALENDA si kwa sababu ya kujua jinsi siku zinavyokwenda bali zaidi kujipanga katika siku zinavyokuja.
Tunapoanza mwaka mpya 2008 sauti ya mzee Chirangi inatuasa sote kuwa tuwe watu wa mipango na utekelezaji. Tuweke mipango yetu ya muda mfupi na mrefu popote tulipo iwe ni katika familia, au katika Chama au Taasisi au Kampuni au Usharika, au Jumuiya yeyote kwa ajili ya maendeleo yetu. Maana ni kweli kuwa usipojua unapoelekea kamwe huwezi kupotea maana popote utakapokuwa utafikiri kuwa umefika.

“ Busara zako, utu wako na hekima zako ni hazina kubwa sana sio kwa familia yako tu bali kwetu sisi sote” Mgeni namba. 228 wa Mzee Chirangi. Mh. H. N. Ole – Mkuu wa Wilaya Musoma, Aug. 2001.

KWA HESHIMA NA SHUKRANI, FAMILIA YA CHIRANGI INAWASILISHA.




Prof. Dr. Sospeter Muhongo
Mdogowe Mzee Mutaragara